Shirika la Yesu
Shirika la Yesu (kwa Kilatini Societas Iesu, kifupi S.J. au S.I. au SJ au SI) ni shirika kubwa la watawa wanaume 15,842 (2018) katika Kanisa Katoliki, lililoenea katika nchi 112 za kontinenti 6.
Wanashirika wanaitwa Wajesuiti na ni maarufu pia kwa elimu yao ya juu katika fani mbalimbali, za kidunia na za kidini.
Historia
haririMwanzilishi wake ni Ignas wa Loyola, Mhispania ambaye alikuwa mwanajeshi. Mwaka 1521 alijeruhiwa vibaya vitani. Alipokaa hospitalini muda mrefu akasikia wito wa Mungu uliobadilisha maisha yake. Kisha kuacha jeshi, akamtolea Bikira Maria upanga wake akawa "Mwanajeshi wa Kiroho". Alifuata kwa juhudi zote maisha ya kiroho na kutunga Mazoezi ya Kiroho ili kuongoza watu wamfuate Yesu Kristo.
Mwaka 1534, Ignas alikusanya vijana sita wakaweka nadhiri za ufukara, useja mtakatifu na utiifu, halafu ile ya kumtii daima Papa.
Kisha kusoma teolojia akapadrishwa. Akakusanya kikundi cha marafiki akiwaongoza kujenga maisha ya kiroho kwa njia ya mazoezi ya pekee. Wote walifuata utaratibu uleule. Kila mwaka walikutana kwa kipindi cha sala, kutafakari na kusoma kilichofuata hatua au mbinu maalumu. Wengi walianza kumfuata na chama chake kikakubaliwa na Papa mwaka 1540.
Shirika la Yesu lilikuwa chombo muhimu sana cha urekebisho wa Kikatoliki kikiwa jumuia ya mapadri iliyoongozwa na "Jenerali" wake akitumia nidhamu ya kijeshi.
Shabaha kuu ilikuwa kutetea Kanisa chini ya Papa.
Kila mwanachama alitakiwa kuwa na elimu ya juu. Hivyo Kanisa Katoliki liliimarika katika teolojia, jambo lililowahi kukazwa zaidi na Waprotestanti.
Mapadri Wajesuiti walifanya hasa kazi ya ualimu wakiunda shule na kufundisha vijana elimu pamoja na upendo kwa Kanisa Katoliki.
Mkazo mwingine ulikuwa kufufua utaratibu wa maungamo. Popote Ulaya Wajesuiti walikuwa washauri hasa wa watawala Wakatoliki. Waliposikiliza ungamo la dhambi zao walipata nafasi nzuri ya kuwapa mawazo na kusababisha hatua za serikali dhidi ya Waprotestanti.
Hivyo kwa athari ya Wajesuiti polepole Uprotestanti ulirudi nyuma katika nchi za Ulaya ambako wakazi wengi walikuwa wameanza kufuata mafundisho ya Martin Luther na Calvin lakini watawala walikuwa bado Wakatoliki.
Papa Fransisko ni wa kwanza kutokea shirika hilo.
Viungo vya nje
haririMafundisho ya Papa Benedikto XVI
hariri- Benedict XVI's Address to the Members of the Society of Jesus, 22 April 2006
- Benedict XVI's Visit to the Pontifical Gregorian University, 3 November 2006
Hati za Wajesuiti
hariri- The Jesuit Ratio Studiorum of 1599 Archived 16 Mei 2008 at the Wayback Machine.
- The Jesuit Mission Press in Japan, 1591–1610 Archived 26 Juni 2003 at the Wayback Machine.
- Letter of the Jesuit Social Justice Secretariat to the leaders of the G8, Julai 2005PDF (98.5 KB)
Tovuti za Wajesuiti sehemu mbalimbali
hariri- The Jesuit Portal – Jesuit Worldwide Homepage
- Directory of Jesuit Websites
- Ignatian wiki Archived 30 Septemba 2020 at the Wayback Machine.
- Jesuit Refugee Service Archived 2 Septemba 2010 at the Wayback Machine.
- Sacred Space: long-running Jesuit daily prayer site Sacred Space, in 20 languages, coordinated by the Jesuits of the Irish Province
Afrika
hariri- Jesuits in East Africa Archived 18 Januari 2019 at the Wayback Machine.
- Jesuits in West Africa
- Jesuits in South Africa Archived 28 Agosti 2008 at the Wayback Machine.
- Jesuits in Zimbabwe Archived 11 Agosti 2018 at the Wayback Machine.
Amerika Kaskazini
hariri- Jesuits in English Canada
- Jesuits in French Canada Archived 23 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.
- United States Jesuit Conference
- Old Catholic (not Roman) Jesuits in the United States Archived 28 Septemba 2009 at the Wayback Machine.
Amerika Kusini
haririAsia-Oceania
hariri- Jesuits in Australia
- Jesuits in Goa, India
- Jesuits in Indonesia
- Finding God in All Things Archived 12 Agosti 2017 at the Wayback Machine. Blogsite on Ignatian Spirituality and Jesuits (in Indonesian)
- Jesuits in the Philippines
- Jesuit universities in the Philippines Archived 19 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
- Jesuits in Malaysia and Singapore
Ulaya
hariri- Jesuits in Britain Archived 11 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- Jesuits in Croatia
- Jesuits in Belgium (North)
- Jesuits in Belgium (South) Archived 3 Oktoba 2011 at the Wayback Machine.
- Jesuits in France
- Jesuits in Germany
- Jesuits in Hungary
- Jesuits in Ireland
- Jesuits in Italy
- Jesuits in Poland
Vyombo vya habari
hariri- The BBC Radio 4 In Our Time programme on 18 Januari 2007 was devoted to the early history and educational role of the Jesuits; the programme's website offers a free podcast and 'listen again' service In Our Time website
- Pray-as-you-go: latest initiative by the British Jesuits, providing daily prayer in MP3 format for use "on the go"
- Documentary by the Society of Jesus Province of Chicago (Windows Media Player) Archived 30 Septemba 2009 at the Wayback Machine.
- Contemporary Jesuits speak about their Jesuit vocation, the vows, and the mission of the Society of Jesus (Real Player) Archived 18 Septemba 2009 at the Wayback Machine.
- Jesuits Saints and Blessed
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shirika la Yesu kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |