Milnacipran, inayouzwa kwa jina la chapa Savella miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa fibromyalgia na mfadhaiko mkubwa. Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.

Milnacipran
Top: (1S,2R)-milnacipran (L-milnacipran)
Bottom: (1R,2S)-milnacipran (D-milnacipran)
Jina la Utaratibu la (IUPAC)
(±)-(1R,2S)-rel-2-(Aminomethyl)-N,N-diethyl-1- phenylcyclopropane-1-carboxamide
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Ixel, Joncia, Savella, Dalcipran, mengineyo
AHFS/Drugs.com Kigezo:Drugs.com
MedlinePlus a609016
Kategoria ya ujauzito B3(AU) C(US)
Hali ya kisheria Prescription Only (S4) (AU) -only (CA) POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo (tembe), kapsuli)
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili 85%
Kufunga kwa protini 13%
Kimetaboliki Ini
Nusu uhai Masaa manane
Utoaji wa uchafu Figo
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe Milnacipran hydrochloride
Data ya kikemikali
Fomyula C15H22N2O 
 YesY(Hiki ni nini?)  (thibitisha)

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, maumivu ya kichwa, shida ya kulala, kuongezeka kwa jasho na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (palpitations). Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kujiua kwa wale walio chini ya umri wa miaka 25, ugonjwa wa serotonini (hali ya kiwango cha juu sana cha serotonini mwilini inayosababisha mshtuko, homa na kuchanganyikiwa), shinikizo la damu kuongezeka, matatizo ya ini, kutokwa na damu, na wazimu. Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi. Dawa hii ni kizuizi cha uchukuaji upya wa serotonin-norepinephrine (SNRI).

Milnacipran iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2009. Ilikataliwa kuidhinishwa barani Ulaya mwaka wa 2009 kutokana na manufaa yake ya kutiliwa shaka. Nchini Marekani, iligharimu takriban dola 420 za Marekani kwa mwezi mmoja kufikia mwaka wa 2021.

Marejeo

hariri