Mirinda
Mirinda ni aina ya vinywaji vya soda vinayotoka nchini Uhispania tangu mwaka 1959. Biashara ya PepsiCola imekuwa ikisambaza Mirinda ulimwenguni tangu mwaka 1970[1].
Jina "Mirinda" linatokana na lugha ya Kiesperanto, likimaanisha "ajabu" au "kushangaza."[2] PepsiCola inaendelea kutangaza na kuuza Mirinda nje ya Marekani, ikishindana na Fanta (kutoka CocaCola) na Crush (kutoka Dr. Pepper Snapple Group).
Majina
haririMirinda inauzwa katika nchi nyingi, na hivyo PepsiCola hurekebisha jina la bidhaa kulingana na mahitaji ya soko. Kwa mfano, Mirinda inaitwa "Sukita" nchini Brazil, "Yedigun" nchini Uturuki, "Slam" nchini Italia, "Sisi" au "Mirindajn" nchini Uholanzi, "Kas" nchini Uhispania, "Frustyle" nchini Urusi, "Mirindan" nchini Ujerumani, "Mirindaj" katika nchi za Scandinavia, na "Sol" katika baadhi ya maeneo nchini Marekani.
Aina
haririMirinda inapatikana kwa aina nyingi na ladha mbalimbali, ikiwa ni pamoja na chungwa, tofaa, tofaa ya kijani, zabibu, limau, stroberi, rasiberi, tikitimaji, pichi, pear, balungi, balungi ya rangi ya waridi, lychee, ndizi, ndizi na chungwa, tikiti, machungwa, nanasi, malai ya rangi ya kijani, vanila, matunda ya rangi ya kijani, zabibu, kuvu ya rangi nyeusi, beri, bia ya mzizi, cola ya machungwa, sarsaparilla, mchanganyiko wa matunda, mchanganyiko wa ladha, toniki, na Club soda. Ladha hizi hutofautiana kutokana na upendeleo wa tamaduni tofauti.
Mirinda pia ina ladha ya "MixIt". Aina hizi za ladha huja katika chupa ambazo zimegawanywa katikati na kuthitaji watu kutikisa chupa ili kuchanganya ladha mbili pamoja. Mirinda inatoa chaguzi za afya pia na aina bila sukari. Mirinda huuzwa katika chupa za glasi, chupa za plastiki, na makopo ya chuma[3].
Historia
haririMirinda ilitengenezwa katika nchi wa Uhispania mwaka 1959 ikawa inapatikana Marekani mwaka 2003. Walipoanza kuoza Mirinda katika Marekani, lebo ya chupa ziliandikwa kwa Kiingereza na Kihispania. Katika nchi tofauti, lebo ya chupa kuna mwandiko kwa lugha ya nchi na pia Kiingereza. Katika mwaka elfu mbili ishirini na tatu biashara ya PepsiCola ilianza kampeni ya matangazo ya kimataifa kwa Mirinda, inaitwa #NoFlavourLikeYourFlavour. Kampeni hii ya utangazaji inaleta rangi mapya kwa lebo kwa kila ladha ya soda. Ilianzishwa nembo mpya na ujumuishaji wa lugha asilia kwenye lebo. Biashara ya PepsiCola ilianza kuonyesha kampeni mpya katika nchini Vietnam na Uthai katika miaka Mei, kisha itaonekana katika Upoland, Romania, Czech (au Jamhuri ya Czech), Ukraini, Hungaria, Kroatia, Gaza/Palestina, Meksiko, Ajentina, Misri, Iraki, Uganada, Ethiopia, Uchina, Pakistan, Kuwait, Qatar, Omani, Bahrain, na Muugano wa Falme za Nchi za Kiarabu ma wengine wengi katika siku zijazo[4].
Wito wa Mirinda kwa nchi za Afrika Mashariki ni “tamu yangu”.
- ↑ "Miranda | PepsiCo.de". web.archive.org. 2012-03-31. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-31. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
- ↑ "Esperanto World Convention . . . . . Fremont, California. . . . . . . . . . . Fremont, Newark, Union City, Hayward . . . . . . . . ". web.archive.org. 2005-02-26. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-02-26. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
- ↑ "Mirinda". Pepsi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
- ↑ PepsiCo. "MIRINDA® UNVEILS VIBRANT NEW VISUAL IDENTITY & 'M'PACTFUL GLOBAL BRAND PLATFORM TO INSPIRE CREATIVITY". www.prnewswire.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-12.