Kiesperanto

Lugha ya kuundwa ya kimataifa iliyotungwa na Bw. Zamenhof

Kiesperanto ni lugha ya kupangwa inayozungumzwa zaidi duniani.Iliundwa na Ludwik Lejzer Zamenhof, Myahudi aliyetoka mjini Białystok, nchini Urusi (siku hizi ni sehemu ya nchi ya Polandi). Alitoa kitabu cha kwanza cha lugha hii mwaka 1887 baada ya kuitengeneza kwa miaka karibu kumi. Nia yake ilikuwa kutengeneza lugha rahisi ili iwe lugha saidizi ya kimataifa, lugha ya pili kwa kila mtu duniani. Waesperanto wengine bado wanataka hiyo, lakini wengine wanapenda kuitumia tu bila nia ya kuieneza duniani kote.

Kiesperanto
Esperanto (eo)
Lugha

Bendera ya Kiesperanto

Asili Poland (Ludwik Lejzer Zamenhof)
Wasemaji

L1 : ~1,000+ (2011)[1]
L2: ~30,000 – 2 milioni (wanaotumia mara kwa mara)

Familia za lugha Lugha bandia
Aina za Awali Proto-Esperanto
Mfumo wa kuandika Alfabeti ya Kilatini
Lugha Rasmi
Lugha rasmi kwa Hakuna rasmi, lakini inatumiwa na Asasi ya Umoja wa Mataifa, UEA (Universal Esperanto Association)
Nambari za Msimbo
ISO 639-1 eo
ISO 639-2 epo
Glottolog espe1235

Waesperanto wanakitumia Kiesperanto kwa ajili ya kukutana na wageni na kujifunza kuhusu nchi na tamaduni nyingine. Siku hizi, maelfu ya watu wanaitumia mara kwa mara ili kuwasiliana na watu popote duniani.

Chunguzi za kitaalamu zimeonyesha kwamba ni rahisi zaidi sana kujifunza Kiesperanto kuliko lugha asilia, na pia kwamba kujifunza Kiesperanto kwanza kunarahisisha kujifunza kwa lugha nyingine.

Sifa za kiisimu

hariri

Kwa kuwa ni lugha ya kupangwa, Kiesperanto hakiko katika familia yoyote a lugha. Maneno yake yanatoka hasa lugha za Kirumi (kama Kifaransa na Kilatini), lakini pia lugha za Kigermaniki (kama Kiingereza na Kijerumani) na lugha za Kislavoni (kama Kirusi na Kipolandi).

Maneno mengi yanaumbwa kwa kuunganisha mzizi wa neno moja na viambishi au kwa kuunganisha mizizi ya maneno mbalimbali. Kwa mfano kuna kiambishi awali "mal-" inayoonyesha kinyume: "bona" ni "-zuri" na "malbona" ni "-baya". Kwa hiyo inawezekana kusema mambo mengi baada ya kujifunza maneno machache tu.

Matamshi na maandishi

hariri

Katika Kiesperanto kuna herufi 28 na sauti 28. Kila herufi inaweza kutamka kwa sauti moja tu, na kila sauti inaandikwa kwa herufi moja tu. Herufi za Kiesperanto ni hizi zifuatazo:

a b c ĉ d e f g ĝ h ĥ i j ĵ k l m n o p r s ŝ t u ŭ v z

Irabu zote (a, e, i, o, u) zinatamka kama kwa Kiswahili.

Kwa upande wa konsonanti, b, d, f, g, h, k, l, m, n, p, r, s, t, v na z zinatamka kama kwa Kiswahili. c inatamka kama ts. ĉ inatamka kama ch. Matamshi ya ĝ yanafanana na matamshi ya j kwa Kiswahili (ni sawasawa na matamshi ya j katika neno la Kiswahili "njia"); j ya Kiesperanto inatamka kama y ya Kiswahili. ĵ inatamka kama j ya Kifaransa (inafanana na sh ya Kiswahili, lakini inatamka na sauti, kama z). ŝ inatamka kama sh. ŭ inatamka kama w; ŭ inatumika baada ya a na e tu, ingawa Zamenhof wenyewe na Waesperanto wengine waiunganisha na irabu yoyote, k.m. "sŭahila" (Kiswahili), "ŭato" (wati), tena jina la herufi yenyewe ni "ŭo"; tofauti kati ya au na ni kwamba au inatamka kwa silabi mbili na kwa silabi moja.

Sarufi

hariri

Nomino (majina) zote zinahitimu kwa kiambishi tawali -o, kwa mfano "arbo" (mti). Wingi wa nomino unahitimu kwa -oj (arboj = miti).

Vivumishi vinahitimu kwa kiambishi tawali -a, kwa mfano "alta" (-refu). Vivumishi kwa kawaida vinawekwa kabla ya nomino inayohusu, lakini pia inaweza kuwa baada yake. Wingi pia unaonyeshwa katika vivumishi kwa harufi "j": altaj arboj = miti mirefu.

Vitenzi vina viambishi tamati mbalimbali:

  • -i inatumika kwa vitenzi-jina (kwa mfano "fari" = "kufanya")
  • -as inatumika kwa njeo ya wakati uliopo (kwa mfano "mi faras" = "ninafanya"
  • -is inatumika kwa njeo ya wakati uliopita (kwa mfano "mi faris" = "nilifanya" au "nimefanya")
  • -os inatumika kwa njeo ya wakati ujao (kwa mfano "mi faros" = "nitafanya")
  • -us inatumika kwa hali a masharti (kwa mfano "mi farus" = "ningefanya")
  • -u inatumika kwa hali ya kuamuru (kwa mfano "faru!" = "fanya!"; "li faru" = "afanye")

Tanbihi

hariri
  1. "Esperanto native Population". Archive.org (kwa Kiesperanto). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2025-02-20.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)

Viungo vya nje

hariri