Mīrjāveh (Farsi میرجاوه) ni mji mdogo wa mkoa wa Sistan na Baluchistan katika Uajemi karibu na mpaka wa Pakistan. Hapa kuna kituo cha mpakani cha pekee cha barabara na reli kati ya Uajemi na Pakistan. Mji wa mpakani upande wa Pakistan unaitwa Taftan sawa na Volkeno yenye jina lileile upande wa Uajemi.

Mirjaveh
Majiranukta: 29°1′28″N 61°27′54″E / 29.02444°N 61.46500°E / 29.02444; 61.46500
Nchi Uajemi
Majimbo Sistan na Baluchistan
Mji wa Mirjaveh

Mji ulikuwa na wakazi 13.590 katika mwaka 2006. Uko kilomita 75 upande wa kusini mashariki wa Zahedan.

Marejeo

hariri