Mkoa wa Sistan na Baluchistan

(Elekezwa kutoka Sistan na Baluchistan)

Sistan na Baluchistan (kaj ‏سيستان و بلوچستان‎) ni moja wa mikoa 30 ya Uajemi. Makao makuu yako mjini Zahedan.

Mahali pa mkoa wa Sistan na Baluchistan katika Uajemi

Mwaka 2006 idadi ya wakazi ilikuwa watu 2,405,742. Mkoa una eneo la 181,785 km² na msongamano wa wakazi 13 kila kilomita ya mraba.

Jiografia

hariri

Mkoa uko katika kusini mashariki ya Uajemi ukipakana na Afghanistan, Pakistan, Ghuba ya Omani (Bahari Hindi) na mikoa jirani ya Khorasan Kusini, Kerman na Hormozgan.

Zahedan yenye wakazi 567,449 (sensa 2006) ni mji mkubwa mkoani. Kaskazini ya mkoa ni eneo la Sistan na kusini ya mkoa ni sehemu ya kiajemi ya Baluchistan.

Mkoa hupokea mvua kidogo kwa wastani milimita 80 kwa mwaka. Sehemu kubwa ya usimbishaji hupatikana kati ya Oktoba na Machi ( mvua milimita 8 - 15) na miezi kati ya Aprili na Septemba ni yabisi yenye usimbishaji wa milimita 0 - 8 pekee.

Halijoto ya wastani ni sentigredi 20.8; mwezi baridi ni Januari yenye wastani ya 7.5 °C na mwezi wa joto ni Julai yenye wastani ya 33.1 °C.

Utawala

hariri

Sistan na Baluchistan huwa na wilaya 8 ambazo ni

Wakazi

hariri

Wakazi walio wengi sana ni Wabaluchi ambao ni jamii kubwa yenye lugha ya pamoja wanaokalia sehemu za Uajemi mashariki, Afghanistan kusini na kusini-magharibi ya Pakistan.

Wengi wao ni Wasunni tofauti na wakazi wengine wa Uajemi walio Washia hasa.

Umaskini ni kubwa mkoani ingawa kuna malighafi kama madini mbalimbali ambazo hazikuanza kuchimbwa bado.