Mishipa ya damu
Mishipa ya damu (ing. blood vessels) ni mabomba ndani ya mwili ambamo damu inasafirishwa pande zote za mwili. Pamoja na moyo inaunda mfumo wa mzunguko wa damu mwilini.
- Ateri ni mishipa inayopeleka damu kutoka moyoni kwenda mwilini.
- Vena ni mishipa inayopeleka damu kuingia moyoni kutoka mwilini.
Ateri huwa nyembamba zaidi kadri zisivyofika mbali na moyo. Mwishoni ni nyembamba sana huitwa aterioli na kuingia katika kapilari ambazo ni vyombo vya damu vyembamba mno zinazolisha seli za mwili moja kwa moja.
Vivyo hivyo vena zinaanza kwa umbo neymbamba upande wa kinyume cha kapilari zikiitwa venuli. Zinaongezeka unene kadri zinavyokuwa karibu zaidi na moyo.
Kwa hiyo mwendo au mzunguko wa damu ni moyo halafu mishipa ya ateri - aterioli - kapilari - venuli - vena hadi moyoni tena.
Ateri na vena zina ganda la musuli zinazokaza na kulegea na hiyvo kusukuma damu iende pale inapotakiwa.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mishipa ya damu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |