Miss South Africa
Miss South Africa ni shindano la urembo la kitaifa nchini Afrika Kusini ambalo huchagua wawakilishi wa Afrika Kusini kushiriki katika mojawapo ya mashindano makubwa manne ya kimataifa ya urembo kama vile Miss Universe.Pia, huchagua mwakilishi mwingine kushiriki katika shindano la kimataifa la Sub-major, Miss Supranational. Shirika la Miss South Africa lilibadilisha mfumo wake wa kuchagua wawakilishi na kuanzisha mfumo wa kisasa mnamo mwaka 2018. Kwa kufuata mbinu yao mpya, Miss World South Africa na Miss Universe South Africa walichaguliwa kama wawakilishi. Kuanzia mwaka 2021 na kuendelea, mshindi wa Miss South Africa atashiriki kwenye Miss Universe na Miss Supranational. Miss Afrika Kusini wa sasa 2024 ni Mia le Roux .Mnamo Mei 11, 2023, Shirika la Miss South Africa lilipoteza leseni yake ya kuandaa shindano la Miss World, na leseni hiyo kuchukuliwa na Carol Bouwer Productions, ambayo sasa itaandaa shindano la Miss World South Africa [1]
Maarejeo
hariri- ↑ "Carol Bouwer is the new Miss World South Africa licence holder", SApeople News, 12 May 2023.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |