Uzuri

(Elekezwa kutoka Urembo)

Uzuri ni sifa ya nafsi, mnyama, mahali, tendo, wazo, neno, tungo, sauti, picha au kitu chochote kinachopendeza.

Anga katika Atacama Desert. Uzuri wa uasilia umekuwa mara nyingi kichocheo cha usanii wa binadamu.
Faili:Kelly, Grace (Rear Window).jpg
Grace Kelly. Sura ya binadamu inaweza kuwa na uzuri mkubwa.
Pambo la maua, Jin Dynasty (11151234 BK), Shanghai, China.
Dirisha la rangi katika kanisa la Notre Dame de Paris, Ufaransa. Katika sanaa ya Kigothi, nuru ilitazamwa ufunuo wa kwanza wa Mungu.
Kuba la Kanisa kuu la Florence. Kuanzia tapo la Renaissance huko Ulaya, ulinganifu na uwiano wa vipimo vilitazamwa vya msingi katika suala la uzuri.

Kimsingi, kwa wanaomuamini Mungu, ni sifa yake ambayo inajumlisha zile za umoja, ukweli na wema, na kujitokeza katika utakatifu wa watu wake.

Kwa namna mbalimbali uzuri unachunguzwa na falsafa, sosholojia, saikolojia n.k. na kulengwa na binadamu tangu zamani za kale, hasa kwa njia ya sanaa za aina mbalimbali. Tangu mtu yupo, hawezi kuridhika na mahitaji ya mwili tu.

Pengine uzuri unategemea utamaduni, lakini mara nyingi unapendeza watu wote.

Mang'amuzi ya "uzuri" mara nyingi yanatokana na utambuzi wa ulinganifu na uasilia, unaomfanya mtu ajisikie salama na kuridhika.

Hata hivyo, kwa kuwa mara kadhaa ni mang'amuzi ya binafsi, mithali ya Kiingereza inasema, "beauty is in the eye of the beholder" ("uzuri umo jichoni mwa mtazamaji")[1]hata pengine ni suala la urithi.[2][3]

Tanbihi

hariri
  1. Gary Martin (2007). "Beauty is in the eye of the beholder". The Phrase Finder. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-30. Iliwekwa mnamo Desemba 4, 2007. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. The Oxford Handbook for Aesthetics
  3. "Denis Dutton: A Darwinian theory of beauty | Video on TED.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-11. Iliwekwa mnamo 2014-09-22.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: