Mitotane
Mitotane, inayouzwa kwa jina la chapa Lysodren miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu saratani ya tezi la adrenali na ugonjwa wa Cushing.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1] Wakati wa matibabu, kundi la homoni za steroidi (corticosteroids) linahitajika mara nyingi.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu, kuhara, kuhisi usingizi na upele.[1] Matatizo yake mengine yanaweza kujumuisha kutokwa na damu kutokana na saratani, uharibifu wa ubongo, na upungufu wa tezi za adrenal. [1] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[2] Dawa hii inafanya kazi kwa kuzuia gamba la adrenal.[3]
Mitotane ilianzishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu mwaka wa 1960.[4] Nchini Uingereza, vidonge 100 vya miligramu 0.5 huigharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £590 kufikia mwaka wa 2021.[3] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 1,100 za Marekani.[5]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Mitotane Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 18 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mitotane (Lysodren) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 18 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 979. ISBN 978-0857114105.
- ↑ Marcello D. Bronstein (1 Oktoba 2010). Cushing's Syndrome: Pathophysiology, Diagnosis and Treatment. Springer Science & Business Media. ku. 156–. ISBN 978-1-60327-449-4.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Lysodren Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 18 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mitotane kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |