Mji Haramu
Mji Haramu ni mtaa ndani ya mji wa Beijing (China) ni eneo la nyumba za makaisari wa China. Familia za kifalme za Ming na Qing ziliishi humo hadi mapinduzi ya 1911.
Watu raia walikataliwa kuingia kabla ya mapinduzi ya China hivyo jina la "mji haramu" lilipatikana. Nje ya ukuta wa mji haramu uko uwanja wa Tiananmen.
Eneo lake ni 720,000 m² kuna majengo 800 yenye vyumba 8,886.
Mji Haramu umeandikishwa katika orodha la UNESCO la Urithi wa Dunia.