Katika takwimu, mkengeuko wastani (kwa Kiingereza "standard deviation") ni kipimo cha kiasi cha tawanyiko ya sampuli ya data. Mkengeuko wastani wa chini unaonyesha thamani za sampuli ya data ni karibu na wastani, ilhali mkengeuko wastani wa juu unaonyesha thamani ni mbali na wastani.

Mkengeuko wastani wa sampuli ya data ya kawaida.


Umeandikwa kwa herufi ya Kigiriki σ au kwa herufi ya Kilatini S


Mkengeuko wastani ni kipimo cha tawanyiko kama muachano au masafa.

Kwa programu ya takwimu R

hariri

Ili mtafute mkengeuko wastani kwa lugha ya programu ya takwimu R mandike :


> SampuliYangu<- c(7, 4, 3, 6, 9, 2, 9, 13, 9, 9)

> sd(SampuliYangu)

[1] 3.381321

Marejeo

hariri
  • Saleh, A. M. E., & Ehsanes, M. (2001). An introduction to probability and statistics. Wiley.
  • Peck, R., Olsen, C., & Devore, J. L. (2015). Introduction to statistics and data analysis. Cengage Learning.