Mkondo wa Benguela

Mkondo wa Benguela ni mkondo wa bahari katika Atlantiki ya Kusini unaotoka katika bahari baridi karibu na Antaktika na kuelekea kaskazini ukipita kwenye pwani la magharibi la Afrika. Mkondo una upana wa 200-3000 km.

Mkondo wa Benguela kati ya mikondo ya Atlantiki ya Kusini
mikondo baridi kwa rangi ya buluu - mikondo ya vuguvugu kwa rangi nyekundu

Mkondo husukuma maji baridi kwenye pwani la Afrika Kusini, Namibia na Angola. Maji yake huwa vuguvugu kiasi jinsi inavyofika kaskazini katika halijoto ya juu zaidi. Karibu na ikweta unabadilika mwelekeo wake na kuingia katika mkondo wa kusini ya ikweta. Sehemu ya maji yake inaingia katika bahari ya Karibi na kulisha mkondo wa ghuba.

Kusini ya rasi ya Afrika mkondo wa Benguela unakutana na maji ya vuguvugu ya mkondo wa Agulhas kutoka Bahari Hindi.

Athira kwa hali ya hewa Namibia

hariri

Ukipita kwenye pwani la Namibia husababisha hali ya hewa kavu sana. Baridi ya mkondo wa Benguela hupoza upepo kutoka kusini-magharibi na kuusababisha kunyesha unyevu wake kama mvua baharini hivyo kuzuia mvua barani. Jangwa la Namib ni tokeo la mazingira haya. Halijoto ya maji kwenye mwambao wa Namibia huwa ni kwenye 15 °C na ukungu hutokea mara kwa mara mwambaoni.