Mkungu
(Terminalia catappa)
Mkungu
Mkungu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Myrtales (Mimea kama mkarafuu)
Familia: Combretaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mkongolo)
Jenasi: Terminalia
Spishi: T. catappa L.

Mkungu (Terminalia catappa) ni mti mkubwa unaopandwa sana katika kanda ya tropiki. Asili yake labda ni Asia ya Kusini lakini hii siyo ya hakika. Jozi za matunda yake (kungu) huliwa sana huko pwani.