Mlango ni muundo unaotumiwa kuzuia na kuruhusu kuingia jengo, gari, n.k.

Mlango wa hifadhi ya taifa huko Washington, Marekani.
Mlango mzuri

Wakati ni wazi, milango inakubali watu, wanyama, hewa au mwanga n.k.

Mlango hutumiwa kudhibiti hali ya hewa, ili ndani kuwe na joto au baridi kuliko nje. Pia hufanywa kama kizuizi kwa kelele.

Pengine watu hufungua na kufungwa milango kama ishara ya faragha.

Milango mingine ina vifaa vya kuzuia watu fulani na kuacha wengine waingie.

Mara nyingine milango hupewa maana ya ibada, na kulinda au kupokea funguo za mlango, au kupewa nafasi ya kufungua mlango inaweza kuwa na umuhimu maalum.