Mnandi-pwani
Jenasi ya ndege wa bahari
Mnandi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mnandi-pwani mkubwa (Fregata minor)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Spishi 5:
|
Minandi-pwani ni ndege wa bahari wa jenasi Fregata, jenasi pekee ya familia Fregatidae. Wana domo refu lenye ncha kwa kulabu, mabawa marefu na mkia wenye panda. Rangi yao ni nyeusi; jike ana tumbo jeupe na dume ana mfuko wa koo mwekundu ambao anaweza kumvimbisha ili kumvutia jike. Ndege hawa hawaogelei na watembea kwa shida, kwa hivyo wako hewani takriban saa zote. Wanaweza kukaa hewani hata zaidi ya wiki moja. Kama shakwe-waporaji, huonekana mara nyingi wakipora mateka kwa ndege wengine, lakini chakula chao hasa ni samaki, ambao huwakamata wakiruka, na kwa kiasi kidogo zaidi makinda ya ndege. Jike hutaga yai moja au mayai mawili juu ya mti au ardhini au juu ya mwamba wa pwani.
Spishi za Afrika
hariri- Fregata aquila, Mnandi-pwani Tai-bahari (Ascension Frigatebird)
- Fregata ariel, Mnandi-pwani Mdogo (Lesser Frigatebird)
- Fregata a. iredalei, Mnandi-pwani wa Aldabra (Aldabra Frigatebird)
- Fregata magnificens, Mnandi-pwani wa Amerika (Magnificent Frigatebird)
- Fregata minor, Mnandi-pwani Mkubwa (Great Frigatebird)
- Fregata m. aldabrensis, Mnandi-pwani wa Komori (Comoros Frigatebird)
Spishi ya bara jingine
hariri- Fregata andrewsi (Christmas Frigatebird)
Picha
hariri-
Mnandi-pwani tai-bahari
-
Mnandi-pwani mdogo
-
Mnandi-pwani wa Amerika
-
Minandi-pwani mkubwa
-
Christmas frigatebird