Moscow Times ni gazeti lililo katika lugha ya Kiingereza na limechapishwa jijini Moscow, Urusi tangu mwaka wa 1992. Usambazaji wa gazeti hili, katika mwaka wa 2008, ulikuwa nakala 35,000. Gazeti hili hutolewa bure kwa pahali ambapo wasomi wanaozungumza Kiingereza huzuru hasa hoteli na mikahawa wanapokula vyakula vyao. Magazeti haya hupatikana ,pia, kwa njia ya kusajili na kampuni na kutumiwa kwa anwani yako. Gazeti hili ,hivi sasa,limeanza kuwa maarufu sana na Warusi wanaozungumza Kiingereza. Hata hivyo halipatikani katika maduka ya magazeti na kulipata unahitaji kuagiza kutoka kampuni kama ilivyoelezwa hapo juu.

Moscow Times
Jina la gazeti Moscow Times
Aina ya gazeti Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1992
Eneo la kuchapishwa Moscow
Nchi Urusi
Mhariri Andrew McChesney
Mmiliki Kampuni ya Ufini ya Sanoma.
Makao Makuu ya kampuni Moscow
Nakala zinazosambazwa 35,000 - katika mwaka wa 2008
Machapisho husika *.The Moscow Times published Russia for Beginners: A Foreigners Guide to Russia
*.The St. Petersburg Times
Tovuti http://www.themoscowtimes.com/

Gazeti hili lilianza kama gazeti la kuchapishwa mara mbili kwa wiki kabla ya kuwa gazeti la kila siku baada ya miezi kadhaa. Gazeti hili lina makao yake makuu katika makao ya zamani ya gazeti la Pravda,likawa gazeti la kwanza la nchi za Magharibi kuchapishwa nchini Urusi.

Mpaka mwaka wa 2005, jarida hili lilimilikiwa na Independent Media, kampuni ya uchapishaji iliyosajiliwa jijini Moscow na inachapisha magazeti kadhaa : gazeti la kila siku la lugha ya Kirusi, Vedomosti, St. Petersburg Times(hili ni gazeti ambalo ni sawa na Moscow Times jijini St. Petersburg) na huchapisha ,pia, majarida mbalimbali maarufu kama FHM, Men's Health na Cosmopolitan katika lugha ya Kirusi. Mwaka uo huo, Independent Media ilinunuliwa na Kundi la Uchapishaji la Kifini,linaloitwa Sanoma.

Mhariri mkuu ni Andrew McChesney, aliyepandishwa hadi cheo hicho mnamo mwezi wa Juni 2006 baada ya kufanya kazi katika vyeo vingine mbalimbali katika kampuni hiyo.

Gazeti hili huchapisha mara kwa mara makala kadhaa ya waandishi maarufu wa Urusi, mara nyingi wao huchukua misimamo pinzani dhidi ya Serikali ya Kirusi na sera zake kwa jumla. Katika mwaka wa 2009, The Moscow Times ilichapisha Russia For Beginners: A Foreigner's Guide to Russia ambalo lilikuwa jarida kwa wageni nchini Urusi lilioandikwa na waandishi waliotoka nchi geni kuishi Urusi. Wanaeleza matukio yaliyowafanyikia walipokuwa wageni nchini Urusi wakilenga kuwasaidia wageni wapya.

Gazeti hili ,na vilevile gazeti dada lake la The St Petersburg Times, linamilikiwa na Shirika la Sanoma ambalo lina makao yake Ufini.

Marejeo

hariri
  1. "About the newspaper" (PDF) Ilihifadhiwa 12 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.. English Media Kit. The Moscow Times..
  2. Richardson, Dan. (2001). The Rough Guide to Moscow. Rough Guides. uk. 56. ISBN 978-1858287003
  3. Charlton, Angela. (2007). Frommer's Moscow & St. Petersburg. John Wiley and Sons. uk. 63. ISBN 978-0764588990
  4. Lawton, Anna. (2004). Imaging Russia 2000: Film and Facts. New Academia Publishing, LLC. uk. 107. ISBN 978-0974493435.
  5. "Russia for Beginners. A Foreigner’s Guide to Russia". The Moscow Times. 3 Machi 2009.

Viungo vya nje

hariri