Mpango wa Miaka kumi kwaajili ya vijana barani Afrika

Bara la Afrika ndio lenye asilimia kubwa ya Vijana duniani ikiwa na zaidi ya Vijana milioni 400 wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 35. Kwa ongezeko hili la vijana barani Afrika ni muhimu kuwa na ukuaji wa uwekezaji kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ili kuboresha maendeleo ya Mataifa ya Afrika.

Umoja wa Afrika umetengeneza sera za maendeleo mbalimbali kwaajili ya bara zima ili kuhakikisha bara zima linanufaika na sera hizo. Sera hizo ni pamoja na mikataba kwa ajili ya vijana wa Afrika, mipango ya miaka kumi kwaajili ya vijana, na Mpango wa uwezeshaji wa vijana wa Malabo. Yote haya yakifanikishwa kupitia programu 2063 za Umoja wa Afrika. [1]

Mpango wa Miaka kumi kwaajili ya vijana una vipaumbele vifuatavyo;

  1. Maendeleo ya elimu na ujuzi
  2. Ajira na ujasiriamali kwa vijana
  3. Uongozi, amani na ulinzi
  4. Afya na haki za uzazi kwa vijana
  5. Kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira

Marejeo

hariri
  1. "Youth Development | African Union". au.int. Iliwekwa mnamo 2022-12-12.