Mpira wa Kikapu Misri

Shirikisho la mpira wa Kikapu nchini Misri Ni Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchi Misri linaloongozwa na baraza la mchezo wa mpira wa vikapu. Ilijiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu FIBA ​​mnamo mwaka 1934.

Historia

hariri

Iilianzishwa mnamo mwaka 1934, na walikuwa wanachama wa FIBA ​​Ulaya, kwa vile ukanda wa FIBA ​​Afrika haukuanzishwa hadi 1961.[1]

Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri zinapatikana kairo.

Timu za wanaume

hariri

Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri lililenga timu ya taifa ya wanaume ya mpira wa vikapu Nchi Misri, na mafanikio yao yakiwemo nafasi ya 9 katika Olimpiki ya Majira ya mwaka 1952, na nafasi yake ya 5 kwenye Mashindano ya Dunia ya mwaka 1950 FIBA. Katika Mashindano ya FIBA ​​Afrika, Misri inashikilia rekodi ya medali 16. Timu ya wanaume ya Misri ilishiriki Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mara saba. Katika mwaka 1984 na mwaka 1988, Misri ilikuja katika nafasi ya 12 katika hafla zote mbili.[2]

Timu ya wanawake

hariri

Timu ya taifa ya mpira wa vikapu ya wanawake ya Misri ilishinda Ubingwa wa FIBA ​​Afrika kwa Wanawake mwaka 1966 na mwaka 1968, na kushika nafasi ya pili mwaka 1970, kama Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu.

Angalia pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Kenyanstar - Telling the Kenyan Story …" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-09-01. Iliwekwa mnamo 2022-09-01.
  2. "Egypt's Basketball eyeing fresh heights - The Egyptian Gazette". archive.ph. 2013-04-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-04-10. Iliwekwa mnamo 2022-09-01.