Mplamu
Mplamu (Prunus spp.) | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mplamu uliotoa maua
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
|
Mplamu ni mti wa jenasi ya Prunus, na nusujenasi ya Prunus. Nusujenasi hii huutofautisha mplamu na nusujenasi nyingine ( pichi, cheri n.k. ) kwenye matawi kwa kuwa na chipukizi la mwisho na machipukizi mengine yametengana ( hayapo kama kundi ), maua yamekaa pamoja moja mapaka matano, na tunda likiwa na mfereji mmoja kuanzia juu mpaka chini, na jiwe dogo.
Matunda ya mplamu au maplamu yaliyokomaa huwa na utando mweupe ambao huyapa muonekano wa bafaru hivi lakini hutoka kwa urahisi. Hii huwa ni nta, kitaalamu epicuticular wax, na utando huo hujulikana kama “nta ya kuchanua”
Nusujenasi Prunus
haririNusujenasi imegawanywa katika sehemu kuu tatu:
- Sektio Prunus (maplamu ya Dunia ya Kale): Majani ya kwenye chipukizi yanajikunja kuelekea ndani; maua 1 – 3 yanakaa pamoja,; matunda ni laini, daima huwa na hupata nta ya ukomavu
- Sektio Prunocerasus (maplamu ya Dunia Mpya): Maua ndani ya chipukizi yanajikunja kwa ndani; maua 3 – 5 yanakaa pamoja; matunda ni laini; daima huwa na hupata nta ya ukomavu.
- Sektio Armeniaca (maaprikoti): Maua ndani ya chipukizi yanajikunja kwa ndani; maua huwa na vikonyo vifupi; matunda laini kama mahameli. Huchukuliwa kamajinasi ndigo inayojitegemea na baadhi ya waandishi.
Spishi
hariri- Sektio Prunus
- Prunus p. cerasifera
- Prunus p. cocomilia
- Prunus p. consociiflora
- Prunus p. domestica
- Prunus p. salicina
- Prunus p. simonii
- Prunus p. spinosa
- Sektio Prunocerasus
- Prunus p. alleghaniensis
- Prunus p. americana
- Prunus p. angustifolia
- Prunus p. hortulana
- Prunus p. maritima
- Prunus p. mexicana
- Prunus p. nigra
- Prunus p. subcordata
- Sektio Armeniaca
- Prunus p. armeniaca
- Prunus p. brigantina
- Prunus p. mandshurica
- Prunus p. mume
- Prunus p. sibirica
Kilimo na matumizi
haririPlamu huwa na ladha ya utamu na/ au uchachu; huku ngozi mara nyingi ikiwa chachu. Huwa na n=maji mengi mna huweza kuliwa na kama lilivyo au kutumika kutengeza jemu na viungo vingine. Shrubati ya plamu inaweza kuchachushwa na kuwa mvinyo wa plamu; kisha huchujwa na makampuni kadhaa huko Uingereza mashariki yalijitokeza kama vile "Slivovitz", 'Rakia", "Tzuica" au "Palinka". Plamu zilizokaushwa pia huwa nzuri kuliwa. Plamu huwa na kemikali kadhaa, zenye matumizi kadhaaa kwenye mwili wa binadamu na sehemu nyingine. Plamu zilizokaushwa na kuwekwa chumvi na kuliwa kama asusa na hufahamika kama salaito au salao. Baadhi ya viungo vilivyokaushwa vya plamu hupatikana huko kwenye maduka na maduka maalumu sehemu mbalimbali duniani kote. Kemikali ya licorice hutumika kuongeza ladha na hutumika kufanya plamu ziwe na ladha ya chumvi na kutumika na vyakula vingine.
Mafuta ya kiini ya plamu kavu hutengenezwa kutoka sehemu ya ndani ya shimo la plamu.
Plamu huwa katika rangi na ukubwa tofauti. Baadhi huwa na nyama ya ndani ngumu kiasi na mengine huwa na nyama laini na yenye rangi ya njano, nyeupe kijani au nyekundu, na ngozi yenye kubadilika vilevile kulingana na rangi ya nyama ya ndani.
Picha
hariri-
Maua
-
Maplamu mtini
-
Maplamu mekundu
-
Maplamu zambarau
-
Maplamu njano (Mirabelle)
-
Prunus cerasifera
-
Prunus salicina
-
Prunus spinosa
-
Prunus americana
-
Prunus angustifolia
-
Prunus maritima
-
Prunus mexicana
-
Prunus nigra
-
Maaprikoti (Prunus armeniaca)
-
Prunus brigantina
-
Prunus mume
-
Prunus sibirica
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mplamu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |