Wikipedia:Umaarufu

(Elekezwa kutoka Msaada:Umaarufu)

Umaarufu wa kichwa au lemma ya makala ni lazima kueleweka.

Wikipedia SI tangazo juu ya mtu yeyote anayeishi au aliyeishi duniani. Hapa unaweza kutumia facebook au tovuti za aina hii. Mambo yanayojadiliwa hapa ni sharti kuwa na umaarufu au umuhimu fulani katika umma.

  • Labda babako au shangazi walikuwa watu muhimu sana katika maisha yako. Ukweli huu hauundi bado umaarufu wa kutosha wa kustahili makala hapa.
  • Ulianzisha jana bendi au klabu mpya. Mnasikia uhakika ya kwamba mtakuwa watu maarufu kabisa. Lakini leo bado hamjafika hata kidogo. Basi bendi au klabu haistahili bado makala ya wikipedia.

Kanuni ya kimsingi kuhusu umaarufu kwenye Wikipedia

Mada (au mtu) inastahili makala kama masharti matatu yanatimizwa:

  • imeshajadiliwa katika jamii kwa kiwango fulani (si mara ya kwanza hapa wikipedia!)
  • katika vyanzo vinavyoweza kutegemewa (si facebook, twita, tovuti ya binafsi tu)
  • tena vyanzo visivyotungwa na wenyewe (si tovuti ya wenyewe, matangazo yao)

Vyanzo, ushuhuda

Habari za watu katika wikipedia zinahitaji kuthibitishwa kwa kutaja ushuhuda na vyanzo.

Kipimo muhimu ni: Je kuna habari kuhusu kichwa (lemma) katika gazeti, kitabu au tovuti (ambayo si tovuti ya mwenyewe) inayotaja jambo linalojadiliwa? Vyanzo vya aina hii vinatakiwa kutajwa ama kwa umbo la tanbihi (footnote) au katika fungu la marejeo, ama kwa kutaja kitabu (jina la kitabu, mwandishi, kampuni iliyokotoa, mwaka wa kuchapishwa, ukurasa alipotajwa), gazeti (pamoja na tarehe, jina la gazeti, mahali pake, jina la makala, tarehe ) au kiungo cha intaneti.

Ukihitaji maelezo marefu zaidi: ujisomee kwa Kiingereza hapa: Wikipedia:Notability


Ukiulizwa kuhusu umaarufu wa makala usikae kimya. Kama mwanawikipedia mwingine ana wasiwasi kuhusu umuhimu wa jambo ataandika kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala yenyewe au kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Usikae kimya, ujibu, ujitetee, onyesha sababu zako.