Lemma

ukarasa wa maana wa Wikimedia

Lemma (gir. λῆμμα, lemma), pia kidahizo, ni neno la kutaja umbo la kimsingi la neno. Latumika hasa kwa majina au vichwa vya makala za kamusi ambako maneno hupangwa kufuatana na a-b-c kwa umbo la kimsingi yaani lemma.

Kwa hiyo mtungaji wa kamusi anahitaji kuamua ni nini umbo la neno ambalo litapatikana :

  • "kiti" (si: viti)
  • "kupiga" (si walipiga).

angry adj 1 -enye hasira, -enye
chuki, -enye hamaki be ~ kasirika. 2 (of a cut, wound)
-enye kupwita. 3 (sea, sky, clouds) -a kutisha,
iliochafuka. angrily adv kwa hasira/ghadhabu
chuki.

Hapo lemma ni "angry" na inaonyeshwa kwa maana tofautitofauti kulingana matumizi tofauti. Umbo la "angrily" limeongezwa kama lemma ndogo.

Lemma katika wikipedia

hariri

Katika wikipedia "lemma" ni sawa na jina la makala. Lemma ya makala hii unayosoma ni "Lemma" jinsi inavyoonekana katika kichwa.

Ni muhimu kuangalia tahajia ya lemma au jina. Maana ukianzisha makala kwa jina fulani unaunda lemma katika mkusanyiko wa data wa wikimedia. Umbo hili ni muhimu baadaye maana wakati mtu anaweka kiunganishi kwa makala ulioyoanzisha anahitaji kurudia lemma hivihivi bila tofauti. Kama lemma "Julius Nyerere" imeanzishwa lazima utumie tahajia hii si "Julius nyerere" ambayo haitambuliwi katika kiunganishi. Hata hovyo inawezekana kuandaa maumba mbadala kwa njia ya vielekezo ("redirect") na kuzihifadhi kama makala za pekee, mfano Mwalimu Nyerere, Mwalimu Julius Nyerere, Julius Kambarage Nyerere ambazo zote zimeandaliwa kuelekeza kwa "Julius Nyerere" iliyoundwa kama lemma.