Msese (Scolopacidae)

Msese
Msese mkia-mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
Familia: Scolopacidae (Ndege walio na mnasaba na sululu)
Jenasi: Limosa
Brisson, 1760
Spishi: L. fedoa (Linnaeus, 1758)

L. haemastica (Linnaeus, 1758)
L. lapponica (Linnaeus, 1758)
L. limosa (Linnaeus, 1758)

Wasese hawa ni ndege wa jenasi Limosa katika familia ya Scolopacidae (kusoma kuhusu wasese wengine tazama Msese (Recurvirostridae)). Ndege hawa wana rangi ya kahawa au kijivu na wakati wa majira ya kuzaa rangi inakuwa nyekundu zaidi. Wana mdomo na miguu mirefu na mdomo ni mnyofu au umepindika juu kidogo. Katika Afrika huonekana kando ya bahari, viziwa au mito ambapo hutafuta chakula kwa kutumia kuingiza mdomo wao katika matope. Hula nyungunyungu, wadudu na lava za wadudu. Hutaga mayai matatu hadi sita ardhini katikati ya manyasi mafupi.


Spishi za Afrika (na Ulaya)Edit

Spishi za AmerikaEdit

PichaEdit