Mdudu
ukarasa wa maana wa Wikimedia
Mdudu (mkubwa dudu pia) kwa lugha ya mitaani ni aina ya mnyama mdogo asiye vertebrata, yaani mnyama bila uti wa mgongo. Wanyama waitwao “wadudu” wana miguu kwa kawaida (k.m. buibui, nge, jongoo au wadudu wa kweli).
Lakini hata wanyama wadogo bila miguu huitwa wadudu kwa lugha ya kawaida, wanyama wadogo sana hasa (chini ya sentimita moja). Hawa huitwa vidudu (k.m. kidudu-dubu) au hata vijidudu (kwa kawaida viumbe vinavyoonekana chini ya hadubini tu) pia.
Tazama pia
haririWadudu wa kweli.
Yote "dudu"?
hariri-
Sisimizi ni mdudu wa kweli
-
Bui-bweha ni buibui mwenye sumu; si mdudu wa kweli lakini angala buibui hawako mbali sana na wadudu katika uainishaji
-
Kidudu-dubu ni mdogo sana, hana uhusiano wa karibu na wadudu wa kweli