Mto Bann Irish: An Bhanna ni mto mrefu katika Ireland ya Kaskazini, ukiwa na kilometa 129 (maili 80). Mto huu huunda njia yake kutoka kona ya kusini mashariki ya jimbo [1] kuelekea pwani ya kazini magharibi, [2] kukoma katikati na kupanuka kuwa Lough Neagh kubwa. Mto huu umecheza sehemu muhimu katika maendeleo ya viwanda katika kaskazini ya Ireland, hasa katika Viwanda vya Taulo . Leo, uvuvi wa Salmoni na Eel ni vipengele muhimu vya kiuchumi ya mto. Mto huu hutumika kama laini ya kugawanya kati ya maeneo ya mashariki na magharibi ya Ireland ya Kaskazini, na kujulikana kma "Mgawanyo wa Bann ". Halmashauri ya miji na biashara "magharibi ya Bann" mara nyingi huonekanakuwa uwekezaji na matumizi ya serikali ya chini kuliko yale ya mashariki. [3] Pia huonekana kama mgawanyiko wa kisiasa na kidini, ambapo Wakatoliki, Nationalists na Republican wengi kuwa katika magharibi, na Waprotestanti na unionist katika mashariki. [4] [5]

Mito ya Ireland

Bann ya Juu

hariri

Bann ya juu huanzia katika Milima ya Mourne katika Kata ya chinina kutiririka ndani ya Lough Neagh katika Bannfoot, kata ya Armagh. Mkondo huu moja ya mito maarufu ya uvuvi katika Ulaya. Karibu Portadown unajiunga na mtaro wa Newry, usiotumika, ambao ulikuwa njia ya kufika kusini ya Bahari Kiayalandi.

Bann ya Chini

hariri
 
Mtazamo wa Mto Bann katika Coleraine na buga kando ya mto kwenye mafuko za mashariki ya mto

Bann ya chini mtiririko kutoka Lough Neagh katika Toome hadi Atlantiki katika Portstewart. Mto huu njia ya maji ambayo ina mitaro na milango tano lkatika maili 38 (51 km) zake. Mto huu ni maarufu katika michezo ya maji, waendesahji wa mashaua huwa na trafiki ndogo. Huwa kama mpaka kati ya kata ya Antrim na kata ya Londonderry. Bandari ya kibiashara pekee katika mto huu ni katika Coleraine. Meli kutoka Bahari ya Londonderryna Bahari ya Belfast za kuhamisha makaa ya mawe na vyuma chakavu.

Angalia Pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. 54°10′01″N 6°04′59″W / 54.167°N 6.083°W / 54.167; -6.083
  2. 55°09′47″N 6°46′05″W / 55.163°N 6.768°W / 55.163; -6.768
  3. Taarifa za BBC
  4. "Uandikaji wa utafiti wa Ireland ya Kaskazini Toleo la 1993, mtandao wa huduma wa CAIN". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-30. Iliwekwa mnamo 2010-01-25.
  5. "Maandishi ya Strabane ". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-21. Iliwekwa mnamo 2010-01-25.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Bann kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.