Mtori
Mtori ni chakula ambacho kinapendwa na Wachagga wengi nao hupenda kukila hasa wakati wa usiku. ingawa leo mijini wengi hupendelea kula wakati wa asubuhi zaidi. Na vilevile ni chakula cha wagonjwa, hasa wale wasioweza kula chakula kigumu. Chakula hiki cha mtori kina asili ya Arusha, Tanzania.[1][2]
Matayarisho ya Mtori
haririUtengenezaji
haririNyama hupikwa mpaka kuwa laini na pia kupata supu ambayo itatumika wakati wa kuponda ndizi. Pia ndizi hupikwa pamoja na vitunguu na nyanya mpaka kuwa laini kabisa. Baada ya hapo maji yakikauka ndizi hizo hupondwa pondwa mpaka kuwa kama ugali. Sasa supu iliyobaki kwenye nyama inachanganywa na ndizi zilizopondwa mpaka kupata kitu kama uji ambao ni mtori, tayari kwa matumizi hasahasa ikiwa bado moto.
Marejeo
hariri- ↑ Kitu Kizuri (kwa Kiingereza). Kitu Kizuri LLC. 2008.
- ↑ Riyamy, Alya Sened (2001). African Gardens: The Cuisine of Zanzibar and the East African Coast (kwa Kiingereza). Riyamy Publications.