ANATORY RWABUDAGA: Alizaliwa mnamo tarehe 27.05.1966, katika kijiji cha Nyamigere, kata ya Kalenge, wilaya ya Biharamulo, mkoa wa Kagera; nchini Tanzania. Alianza elimu ya msingi mnamo mwaka 1977, s/m Nyamigere, hadi 1983. Alienda sekondari (1984-1987) City High School iliyoko mkoani Dodoma. Amefanya kazi mbali mbali, ikiwa ni pamoja na revenue collector ngazi ya kijiji. Ameoa na ana watoto 8. Anaishi Nyakanazi, kata ya Lusahunga.