Ubaguzi wa kiumri
(Elekezwa kutoka Mtumiaji:Bennforty/ Ubaguzi wa kiumri)
Ubaguzi wa kiumri ni ubaguzi dhidi ya mtu binafsi au vikundi vya watu kwa misingi ya umri wao.[1] Hii inaweza kuzungumzwa tofauti katika nyanja za kijamii, kisiasa na hata katika nyanja mbali mbali za kiuchumi. Msemo huu ulianzishwa mwaka 1976 na Robert Neil Butler kuelezea ubaguzi juu ya watu wazima (wazee), na kwakuzingatia ubaguzi wa kijinsia na ubaguzi wa rangi, Butler alifafanua "umri" kama mchanganyiko wa vipengele vitatu vilivyounganishwa. Hapo awali ilitambuliwa haswa kwa wazee, uzee, na mchakato wa kuelekea uzeeni. Vitendo vya kibaguzi dhidi ya wazee viliendelezwa zaidi na mazoea na sera za kitaasisi zinazoeneza dhana potofu kuhusu wazee.[2]
Marejeo
hariri- ↑ "Ageism and Aging". www.achca.org. Iliwekwa mnamo 2023-03-12.
- ↑ Karlsson, Carl-Johan (2021-07-07). "What Sweden's Covid failure tells us about ageism". Knowable Magazine | Annual Reviews (kwa Kiingereza). doi:10.1146/knowable-070621-1.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ubaguzi wa kiumri kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |