Clophas Flavian Idd alizaliwa tarehe 10/10/1990 katika Kijiji cha Ngulu, Kata ya Kwakoa, Tarafa ya Jipe Ndea, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania.

Wasifu wa Clophas Flavian Idd kwenye elimu.

.Mwaka 1998-2004 Alisoma shule ya

Msingi Ngulu.

.Mwaka 2005-2008 Alisoma Kifaru

Sekondari iliyopo Wilaya ya Mwanga mkoani 
Kilimanjaro.

.Mwaka 2008 Alisoma Chuo Cha

Kompyuta Dar es Salaam tawi la 
Dodoma (UCC).

.Mwaka 2011-2012 Alisoma Chuo Cha

Uandishi wa Habari Morogoro 
(MSJ)ngazi ya Cheti(Astashahada).

.Mwaka 2012-2014 Alisoma Chuo cha

Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) 
(Shahada).
  • Sehemu za Kazi alizofanya

.Clophas Flavian Idd ni Mwandishi

wa Habari nchini Tanzania na 
ameshawahi kufanya Kazi katika 
sehemu zifuatazo....

.Mwaka 2013-2015 alikuwa Mhariri

na Msimamizi wa vipindi katika 
kituo cha Radio Okoa Fm kilichopo 
mkoani Morogoro nchini Tanzania. 
Radio hiyo inamilikiwa na 
Mchungaji anayeitwa Francis 
Katengu.

.Mwaka 2016 Alifanya kazi Kama

Mwakilishi (reporter) kutoka 
mkoani Morogoro wa Kituo Cha East Africa Radio cha Dar es Salaam.

.Mwaka 2017-2018 Alifanya kazi kazi katika kituo Cha Radio Ukweli Fm Morogoro nchini Tanzania, Kama Mhariri wa habari, na Masimamizi wa vipindi. Kituo hiki kinamilikiwa na Jimbo katoliki Morogoro.

.Mwaka 2019---- Anafanya kazi katika

Televisheni ya ITV kama mpiga picha iliyopo nchini 
Tanzania, pia ni mwakilishi (Reporter) wa East Africa Television na East Africa Radio mkoa wa Morogoro.