Mtumiaji:Joeangatia/Stiff-person syndrome
Sindromu ya mtu mgumu | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Faili:Kifundo cha mkono cha mtu mwenye Sindromu ya mtu mgumu Kifundo cha mkono huku amekunja ngumi | |
Kundi Maalumu | Nyurolojia |
Dalili | Misuli migumu, mikazo ya misuli, maumivu[1][2] |
Matatizo | Kukaa vibaya, kuvunjika kwa mfupa, kuanguka mara kwa mara, lhyperlordosis ya kiuno[1][3] |
Muda wa kawaida wa kuanza kwake | 20 to 60[2] |
Muda | Kuzidi kuzorota kwa kasi[2] |
Aina | Klasiki, sio kamili, encephalomyelitis inayoendelea pamoja na ugumu na myoklonus (PERM)[2] |
Visababishi | Haijulikani, autoimmune (kingamwili kuushambulia mwili) [1] |
Njia ya kuitambua hali hii | Kulingana na dalili na kuungwa mkono na vipimo vya damu na elektromiografia[2] |
Utambuzi tofauti | Ugonjwa wa Parkinsons, ugonjwa wa sclerosis nyingi, ugonjwa fibromyalgia, ugonjwa wa kisaikolojia, wasiwasi nyingi[1] |
Matibabu | Diazepam, baclofen, gabapentin, immunoglobulin ya mishipa[1][4] |
Utabiri wa kutokea kwake | Huwa mbaya mara nyingi[4][5] |
Idadi ya utokeaji wake | Nadra[3] |
Sindromu ya mtu mgumu (Stiff-person syndrome) ni ugonjwa wa nyurolojia unaojulikana na misuli ngumu na mkazo wa ghafula wa msuli ambao huendelea kuwa mbaya zaidi muda unapoendelea kusonga.[3][1] Unaathiri kimsingi kiwiliwili, mikono na miguu.[1] Mikazo ya ghafula wa misuli inaweza kuchochewa na sauti, mguso, au hisia.[3] Matatizo yake yanaweza kujumuisha kukaa vibaya, kuvunjika kwa mifupa, maumivu sugu ya muda mrefu, na kuanguka mara kwa mara.[3][1][4]
Katika hali nyingi sababu zake huwa hazijulikani, ingawa inaaminika kwamba hilo linahusishwa na autoimmune (yaani, mfumo wa kingamwili kuushambulia mwili kwa bahati mbaya).[1] Kuna kesi nyingi zinahusishwa na hali zingine za kingamwili kuushambulia mwili, kama vile kisukari cha aina ya 1.[5] Katika hali zisizo za kawaida hutokea kama sindromu ya paraneoplastiki.[4][5] Utambuzi wake mara nyingi hufanyika kwa kupata viwango vya juu sana vya kingamwili na pia asidi ya glutamic decarboxylase (GAD) katika damu au maji ya uti wa ubongo.[1][4] Electromiografia inaweza pia kuwa muhimu sana.[3]
Dalili zake zinaweza kutibiwa kwa dawa kama vile diazepam, baclofen, au gabapentin.[1] Immunoglobulin ya mishipa au plasmapheresis (yaani, kuondoa plasma katika mwili kwa kutoa damu, kuitenganisha iwe plasma na seli, kisha kurudisha seli kwenye mkondo wa damu) pia inaweza kusaidia. [1][4] Kwa ujumla husababisha aina duni ya maisha, kumfanya mtu kuwa na unyogovu au wasiwasi kubwa mara nyingi kama matokeo yake.[4][5] Matarajio ya maisha pia hupunguka mno.[5]
Sindromu ya mtu mgumu ni nadra, na hutokea kwa karibu mtu mmoja kati ya milioni.[4] Huanza mara nyingi kati ya umri wa miaka 20 na 60, ingawa inaweza kutokea kwa watoto kwa njia isiyo ya kawaida.[2] Wanawake huathiriwa mara mbili zaidi kuliko wanaume.[1] Hali hiyo ilielezewa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1956 na Frederick Moersch na Henry Woltman.[2]
Marejeleo
hariri- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 "Stiff-Person Syndrome | National Institute of Neurological Disorders and Stroke". www.ninds.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Desemba 2022. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "NIH2022" defined multiple times with different content - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 Muranova, A; Shanina, E (Januari 2022). "Stiff Person Syndrome". PMID 34424651.
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 "Stiff person syndrome - About the Disease - Genetic and Rare Diseases Information Center". rarediseases.info.nih.gov (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Novemba 2022. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "GARD2022" defined multiple times with different content - ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 4.6 4.7 Ortiz, JF; Ghani, MR; Morillo Cox, Á; Tambo, W; Bashir, F; Wirth, M; Moya, G (9 Desemba 2020). "Stiff-Person Syndrome: A Treatment Update and New Directions". Cureus. 12 (12): e11995. doi:10.7759/cureus.11995. PMID 33437550.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "Ort2020" defined multiple times with different content - ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Hadavi, S; Noyce, AJ; Leslie, RD; Giovannoni, G (Oktoba 2011). "Stiff person syndrome". Practical neurology. 11 (5): 272–82. doi:10.1136/practneurol-2011-000071. PMID 21921002.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "Had2011" defined multiple times with different content