''''''Julius Mahundi'''''' alizaliwa mnamo mwaka 1984, Novemba 28 katika kijiji cha Ngelenge Manda kandokando ya ziwa Nyasa. Jina lake la utoto alijulikana kama Lipyana, neno la Kimanda linalomaanisha Huruma ya Mungu. Yeye ni Mtoto wa sita kuzaliwa katika familia ya Mzee Charles Mahundi yenye watoto nane.

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Ngelenge kuanzia mwaka 1994 hadi 2000 na mwaka 2001 alijiunga na shule ya sekondari ya Manda.