Mtumiaji:Kipala/Wanglia saksoni

Waanglia-Saksoni (Anglo-Saxon) walikuwa Wagermanik wenye asili katika Ujerumani ya Kaskazini ya leo waliohamia Uingereza wakati wa karne ya 5 na 6 BK na kuwa wenyeji. wanatazamiwa kama mababu wa Waingereza wa leo. Jina linaonyesha kwamba walianza kama mchanganyiko wa makabila mbalimbali maana "Anglia" ni sehemu ya jimbo la Schleswig-Holstein ya leo na Wasaksonia walikalia maeneo ipande wa kusini-magharibi kutoka kule (kuanzia Saksonia Chini, Westfalia hadi Uholanzi na pwani la kaskazini ya Ufaransa ya leo).

Hadi mwaka 400 kisiwa kikubwa cha Britania (Great Britain) kilikaliwa na makabila wenye lugha za Kikelti. Kusini cha Britania ilikuwa sehemu ya Dola la Roma; Waroma walitawala juu ya Wakelti wenyeji waliojulikana kama Wabritania na wengi wao walizoa utamaduni mwenye mchanganyiko kati ya ule wa Kiroma na ule wa Kikelti. Mwaka 401 serikali ya Roma iliondoa jeshi lake Britania kwa sababu lilihitajika Italia. Sasa Wabritania wa Kiroma walishambuliwa kutoka Uskoti (kaskazini ya Britania). Hivyo waliwakaribisha Wasaksoni kutoka ng'ambo ya bahari kuja Britania wakawaahidi eneo la kukalia na chakula kwa msaada wa kutetea wananchi dhidi ya Waskoti[1]. Baada ya muda mfupi Wasaksoni hawakuridhika tena na malipo yao na vita ilitokea ambako Wasaksoni walipanusha eneo waliloshika. Vikundi vingine vya Wagermanik walifuata wakivuka Bahari ya Kaskazini na kuvamia Britania. Uvamizi huu uliendelea katika karne ya 5 na ya 6.

Mnamo mwaka 600 sehemu kubwa za Uingereza ya leo ilishikwa na makabila ya Wagermanik, hasa Waanglia na Wasaksoni. Katika mikoa kadhaa kwenye pwani la mashariki walifika pia watu kutoka Denmark na Norwei waliounda madola yao.

Wenyeji asilia walianza kutumia lugha ya mabwana wapya, wengine walihamia maeneo ya mashariki ya Welisi, Cornwall yaliyotawaliwa bado na Wakelti na Gallia (Ufaransa leo).

Kutokana na mchanganyiko huu ulitokea utamaduni wa Kianglia-Kisaksoni. Lugha yao inayoitwa "Kisaksoni cha kale" imekuwa msingi wa lugha ya Kiingereza cha baadaye. Waanglia-Saksoni walifika Britania wakiwa na dini yao asilia lakini kisiwani waligeukia Ukristo.

Waanglia-Saksoni walishambuliwa tena na tena na Waviking wa Skandinavia walioanza kushika maeneo kwenye pwani la mashariki. Katika mapigano haya wafalme wao walitafuta usaidizi wa Wanormandi katika kaskazini ya Ufaransa.

Mwaka 1066 mtemi William Mshindi (William the Conqueror) wa Normandi alivamia Britania na kushinda jeshi la Waanglia-Saksoni akawa mfalme William I wa Uingereza. Wavamizi Wanormandi walikuwa mabwana wapya wa Britania ya kusini wakaendelea kushika maeneo yote ya Waanglia-Saksoni na kutawala kama tabaka ya makabaila. Kwa karne za kwanza baada uvamizi Kifaransa cha mabwana wapya kilikuwa lugha ya milki lakini polepole Wanormandi walizoea lugha ya watawaliwa waliopokea pia maneno mengi kutoka Kifaransa chao. Toleo la mchanganyiko huu ni lugha ya Kiingereza ambayo ni lugha ya Kigermanik yenye maneno mengi ya asili ya Kilatini-Kifaransa.

  1. Gildas: On The Ruin of Britain (De Excidio Britanniae), §23 online hapa