Rhine Kaskazini-Westfalia

Rhine Kaskazini-Westfalia (kwa Kijerumani: Nordrhein-Westfalen, NRW) ni moja kati ya majimbo makubwa ya shirikisho la Ujerumani. Lipo magharibi mwa Ujerumani na idadi ya wakazi ni takriban 18,033,000 waishio katika Jimbo hili: ndilo linaloongoza nchini kwa idadi ya watu.

Rhine Kaskazini-Westfalia, Germany
Ramani ya jimbo la Rhine Kaskazini-Westfalia.
bendera ya Rhine Kaskazini-Westfalia

Mji wake mkuu ni Düsseldorf, lakini mji mkubwa ni Köln (Cologne).

Wilaya za Rhine Kaskazini-Westfalia

hariri

Rhine Kaskazini - Westfalia imegawanyika katika sehemu tano (mikoa ya kiserikali):

Historia ya Rhine Kaskazini-Westfalia

hariri

Jimbo jinsi lilivyo lilianzishwa 1946/1947 na Waingereza walipotawala sehemu ya Ujerumani baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Serikali ya kijeshi ya Kiingereza kwa Ujerumani iliunganisha 1946 mikoa miwili ya Prussia kuwa jimbo jipya baada ya kufutwa kwa Prussia yenyewe iliyowahi kuwa jimbo kubwa kabisa katika Ujerumani. Mikoa hiyo ya Kiprussia ya awali ilikuwa Westfalia na sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Rhine. Washindi wa vita kuu waliwahi kugawa mkoa wa Rhine na kaskazini iliwekwa chini ya Uingereza lakini kusini chini ya utawala wa Ufaransa. Maungano ya Westfalia na Rhine-Kaskazini yalipanuliwa 1947 kwa kuingiza mle jimbo la awali la Lippe. Jimbo jipya kilichokuwa kiumbe cha Waingereza kilikuwa kati ya majimbo 10 yaliyoanzisha mwaka 1949 Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.

Miji ya Rhine Kaskazini-Westfalia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons


 
Majimbo ya Ujerumani
 
Baden-WürttembergBavaria (Bayern)BerlinBrandenburgBremenHamburgHesse (Hessen)Mecklenburg-Pomerini Magharibi (Mecklenburg-Vorpommern)Saksonia Chini (Niedersachsen)Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)Saar (Saarland)Saksonia (Sachsen)Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)Schleswig-HolsteinThuringia (Thüringen)
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rhine Kaskazini-Westfalia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.