Mtumiaji:Lucas559/Bulimia nervosa

Lucas559/Bulimia nervosa
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuTaaluma ya tiba ya magonjwa ya akili, saikolojia ya kimatibabu
DaliliKula chakula kingi kwa kipindi cha muda mfupi na kufuatiwa na kutapika au utumiaji wa dawa za kuharisha, mara nyingi uzani wa mwili huwa wa kawaida [1]
VisababishiSababu za Kijenetiki na za kimazingira[1][2]
Njia ya kuitambua hali hiiKulingana na historia ya kimatibabu ya mtu[3]
Utambuzi tofautiAnoreksia, ugonjwa wa kula kupita kiasi, ugonjwa wa Kleine-Levin, ugonjwa wa kutotulia kihisia[3]
MatibabuTiba ya utambuzi wa tabia[1][4]
DawaVizuizi vya Selective serotonin reuptake, dawa ya mfadhaiko ya tricyclic[2][5]
Utabiri wa kutokea kwakeNusu ya watu hupona katika muda wa zaidi ya miaka 10 wakiwa chini ya matibabu[2]
Idadi ya utokeaji wakeIliwaathiri watu milioni 3.6 (mwaka wa 2015)[6]

Bulimia nervosa, inayojulikana pia kama bulimia, ni ugonjwa wa kula unaojulikana kwa dalili zake za ulaji wa kupita kiasi unaofuatiwa na uondoaji wa chakula mwilini kwa makusudi.[1] Ulaji wa kupita kiasi unamaanisha kula kiasi kingi cha chakula kwa kipindi cha muda mfupi,[1] Uondoaji wa chakula mwilini hufanywa kwa kutapika au kuchukua dawa za kuharisha.[1] Jitihada zingine za kupunguza uzito zinaweza kujumuisha matumizi ya dawa za diuretiki, vichocheo, kutokunywa maji, au kufanya mazoezi kupita kiasi.[1] [2] Watu wengi wenye bulimia wana uzani wa kawaida.[7] Kujilazimisha kutapika kunaweza kusababisha ngozi kuwa nene kwenye vifundo na kuvunjika kwa meno.[1] Bulimia mara nyingi huhusishwa na matatizo mengine ya akili kama vile unyogovu, wasiwasi nyingi na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya au pombe.[1] Pia kuna hatari kubwa ya kujiua na kujidhuru.[8]

Bulimia ni ugonjwa unaotokea zaidi kati ya watu ambao wana jamaa wa karibu walio na ugonjwa huo.[1] Asilimia ya hatari ambayo inakadiriwa kutokana na jeni ni kati ya asilimia 30% na 80%.[2] Sababu zingine za hatari za ugonjwa huu ni pamoja na mfadhaiko wa kisaikolojia, shinikizo la kitamaduni la kufikia aina fulani ya mwili, kutojithamini na unene wa kupita kiasi.[1][2] Kuishi katika jamii inayohamasisha ufuataji wa lishe maalumu na kuwa na wazazi ambao wana wasiwasi kuhusu uzani pia ni hatari.[2] Utambuzi wake unategemea historia ya matibabu ya mtu;[3] hata hivyo, hili ni gumu, kwani kwa kawaida watu huwa wasiri kuhusu tabia zao za ulaji wa kupita kiasi na uondoaji wa chakula mwilini kwa makusudi.[2] Isitoshe, utambuzi wa anoreksia nervosa huchukua nafasi ya kwanza kuliko ile ya bulimia.[2] Matatizo mengine kama hayo ni pamoja na ugonjwa wa kula kupita kiasi, ugonjwa wa Kleine-Levin na ugonjwa wa kutotulia kihisia.[3]

Tiba ya utambuzi wa tabia ndiyo matibabu makuu ya bulimia.[1][4] Dawa za kuzuia mfadhaiko za kizuizi cha selective serotonin reuptake (SSRI) au aina za dawa za mfadhaiko za tricyclic zinaweza kuwa na manufaa ya kawaida.[2][5] Ingawa matokeo zinapotumiwa kutibu bulimia kwa kawaida ni bora kuliko ya wale walio na anoreksia, hatari ya kutokea kwa kifo miongoni mwa wale walioathiriwa ni kubwa kuliko ile ya watu kwa ujumla.[8] Ukifika miaka 10 baada ya kupokea matibabu, karibia asilimia 50% ya watu huwa wamepona kabisa.[2]

Ulimwenguni, bulimia ilikadiriwa kuathiri watu milioni 3.6 mwaka wa 2015.[6] Takribanasilimia 1% ya vijana wanawake wana bulimia kwa kipindi cha wakati fulani na karibia asilimia 2% hadi 3% ya wanawake wana hali hiyo katika kipindi cha wakati fulani katika maisha yao.[8] Hali hiyo haipatikani sana katika nchi zinazoendelea.[2] Bulimia ina uwezekano wa kutokea mara tisa zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.[3] Miongoni mwa wanawake, viwango vyake ni vya juu zaidi kwa vijana watu wazima.[3] Bulimia ilitajwa na kuelezewa kwanza na daktari wa akili wa Uingereza Gerald Russell mwaka wa 1979.[9][10]

Marejeo

hariri
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 "Bulimia nervosa fact sheet". Office on Women's Health. Julai 16, 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 19, 2015. Iliwekwa mnamo Juni 27, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 Hay PJ, Claudino AM (Julai 2010). "Bulimia nervosa". BMJ Clinical Evidence. 2010: 1009. PMC 3275326. PMID 21418667.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 American Psychiatric Association (2013). Diagnostic and Statistical Manual of Mental Disorders (tol. la Fifth). Arlington, VA: American Psychiatric Publishing. ku. 345–349. ISBN 978-0-89042-555-8.
  4. 4.0 4.1 Hay P (Julai 2013). "A systematic review of evidence for psychological treatments in eating disorders: 2005-2012". The International Journal of Eating Disorders. 46 (5): 462–9. doi:10.1002/eat.22103. PMID 23658093.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 McElroy SL, Guerdjikova AI, Mori N, O'Melia AM (Oktoba 2012). "Current pharmacotherapy options for bulimia nervosa and binge eating disorder". Expert Opinion on Pharmacotherapy. 13 (14): 2015–26. doi:10.1517/14656566.2012.721781. PMID 22946772.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 Vos T, Allen C, Arora M, Barber RM, Bhutta ZA, Brown A, na wenz. (Oktoba 2016). "Global, regional, and national incidence, prevalence, and years lived with disability for 310 diseases and injuries, 1990-2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1545–1602. doi:10.1016/S0140-6736(16)31678-6. PMC 5055577. PMID 27733282.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Bulik CM, Marcus MD, Zerwas S, Levine MD, La Via M (Oktoba 2012). "The changing "weightscape" of bulimia nervosa". The American Journal of Psychiatry. 169 (10): 1031–6. doi:10.1176/appi.ajp.2012.12010147. PMC 4038540. PMID 23032383.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 8.0 8.1 8.2 Smink FR, van Hoeken D, Hoek HW (Agosti 2012). "Epidemiology of eating disorders: incidence, prevalence and mortality rates". Current Psychiatry Reports. 14 (4): 406–14. doi:10.1007/s11920-012-0282-y. PMC 3409365. PMID 22644309.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Russell G (Agosti 1979). "Bulimia nervosa: an ominous variant of anorexia nervosa". Psychological Medicine. 9 (3): 429–48. doi:10.1017/S0033291700031974. PMID 482466.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Palmer R (Desemba 2004). "Bulimia nervosa: 25 years on". The British Journal of Psychiatry. 185 (6): 447–8. doi:10.1192/bjp.185.6.447. PMID 15572732.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)