Mtumiaji:Lucas559/Kukoma hedhi

Lucas559/Kukoma hedhi
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuMagonjwa ya wanawake
DaliliKutoona vipindi vya hedhi kwa mwaka[1]
Miaka ya kawaida inapoanzaUmri wa miaka 49 na 52[2]
VisababishiKwa kawaida ni mabadiliko ya asili, upasuaji unaoondoa ovari, baadhi ya aina za Tibakemikali[3][4]
MatibabuHakuna, mabadiliko ya mtindo wa maisha[5]
DawaTiba ya homoni ya kukoma hedhi, clonidine, gabapentin, vizuizi vya kuchagua upya vya serotonini[5][6]

Kukoma hedhi (Menopause), pia inajulikana kama climacteric, ni wakati katika maisha ya wanawake wengi ambapo hedhi hukatika kabisa, na hawawezi tena kuzaa watoto. Kukoma hedhi kwa kawaida hutokea kati ya umri wa miaka 49 na 52.[2] Wataalamu wa kimatibabu mara nyingi hufafanua kukoma hedhi kuwa kumetokea wakati mwanamke hajavuja damu ya hedhi kwa mwaka mmoja. Hali hii inaweza pia kufafanuliwa kwa kupungua kwa uzalishaji wa homoni katika ovari.[7] Kwa wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa uterasi lakini bado wana ovari, kukoma hedhi kunaweza kuzingatiwa kuwa kulitokea wakati wa upasuaji au wakati viwango vyao vya homoni vilipungua.[7] Kufuatia kuondolewa kwa uterasi, dalili kawaida huonekana mapema, kwa wastani wa miaka 45.[8]

Katika miaka kabla ya kukoma hedhi, hedhi ya mwanamke kwa kawaida huwa isiyo ya kawaida,[9] ambayo ina maana kwamba vipindi vinaweza kuwa virefu au vifupi kwa muda au kuwa vyepesi au vizito zaidi katika kiasi cha mtiririko.[9] Wakati huu, wanawake mara nyingi hupata joto kali. Hili kwa kawaida hudumu kutoka sekunde 30 hadi dakika kumi, na linaweza kuhusishwa na kutetemeka, kutokwa na jasho na uwekundu wa ngozi.[9] Mara nyingi joto kali huacha kutokea baada ya mwaka mmoja au miwili. Dalili zingine zinaweza kujumuisha ukavu wa uke, shida ya kulala usingizi na mabadiliko ya hisia. Ukali wa dalili hutofautiana kati ya wanawake.[10] Ingawa kukoma hedhi mara nyingi hufikiriwa kuhusishwa na ongezeko la ugonjwa wa moyo, hili hasa hutokea kutokana na kuongezeka kwa umri na halina uhusiano wa moja kwa moja na kukoma hedhi.[10] Katika baadhi ya wanawake, matatizo yaliyokuwapo kama vile hali ya ukuaji wa tishu za mfuko wa uzazi nje ya mfuko wa uzazi (Endometriosisi) au hedhi yenye uchungu yataboreka baada ya kukoma hedhi.[10]

Kukoma hedhi kwa kawaida ni badiliko la asili, kwani ovari hupungua polepole kadiri umri unavyosonga.[11] Hili linaweza kutokea mapema kwa wale wanaovuta tumbaku. [12] Sababu nyingine ni pamoja na upasuaji ambao huondoa ovari zote mbili au aina fulani za tibakemikali.[3] Katika kiwango cha kisaikolojia, kukoma hedhi hutokea kwa sababu ya kupungua kwa uzalishaji wa ovari homoni za estrojeni na projesteroni. Ingawa kwa kawaida haihitajiki, utambuzi wa kukoma hedhi unaweza kuthibitishwa kwa kupima viwango vya homoni katika damu au mkojo. Kukoma hedhi ni kinyume cha kupata hedhi (menarche), wakati ambapo hedhi ya msichana huanza.[13]

Kwa kawaida, hali hii haihitaji matibabu maalumu.[5] Dalili zingine, hata hivyo, zinaweza kuboreshwa kwa matibabu.[5] Kwa kuzingatia joto kali wakati huu, mara nyingi hupendekezwa kuepuka kuvuta sigara, kafeini na pombe.[5] Kulala katika chumba baridi na kutumia feni kunaweza kusaidia.[5] Dawa zifuatazo zinaweza kusaidia: tiba ya homoni ya kukoma hedhi (MHT), clonidine, gabapentin au vizuizi vya kuchagua upya vya serotonini.[5][6] Mazoezi yanaweza kusaidia kusuluhisha shida za kulala. [5] Ingawa MHT ziliagizwa mara kwa mara, sasa zinapendekezwa tu kwa wale walio na dalili muhimu, kwa kuwa kuna wasiwasi kuhusu madhara yake. Ushahidi wa ubora wa juu wa ufanisi wa dawa mbadala haujapatikana. Kuna ushahidi wa awali kuhusu ufanisi wa matumizi ya phytoestrogens.[14]


Marejeleo

hariri
  1. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Def
  2. 2.0 2.1 Takahashi TA, Johnson KM (Mei 2015). "Menopause". The Medical Clinics of North America. 99 (3): 521–34. doi:10.1016/j.mcna.2015.01.006. PMID 25841598.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Con
  4. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Ca
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 5.6 5.7 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Tx
  6. 6.0 6.1 Krause MS, Nakajima ST (Machi 2015). "Hormonal and nonhormonal treatment of vasomotor symptoms". Obstetrics and Gynecology Clinics of North America. 42 (1): 163–79. doi:10.1016/j.ogc.2014.09.008. PMID 25681847.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 Sievert, Lynnette Leidy (2006). Menopause : a biocultural perspective (tol. la [Online-Ausg.]). New Brunswick, N.J.: Rutgers University Press. uk. 81. ISBN 9780813538563. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2017.
  8. International position paper on women's health and menopause : a comprehensive approach. DIANE Publishing. 2002. uk. 36. ISBN 9781428905214. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2017.
  9. 9.0 9.1 9.2 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Sym
  10. 10.0 10.1 10.2 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named PubMed2013
  11. Suster, David; Liu, Martina Z.; Lin, Douglas I. (2019). "3. Benign diseases of the ovary". Katika Zheng, Wenxin; Fadare, Oluwole; Quick, Charles Matthew; Shen, Danhua; Guo, Donghui (whr.). Gynecologic and Obstetric Pathology (kwa Kiingereza). Juz. la 2. Springer: Springer. uk. 96. ISBN 978-981-13-3018-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Agosti 2022. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2022.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Warren, volume editors, Claudio N. Soares, Michelle (2009). The menopausal transition : interface between gynecology and psychiatry (tol. la [Online-Ausg.]). Basel: Karger. uk. 73. ISBN 978-3805591010. {{cite book}}: |first= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  13. Wood, James. "9". Dynamics of Human Reproduction: Biology, Biometry, Demography. Transaction Publishers. uk. 401. ISBN 9780202365701. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2017.
  14. Franco OH, Chowdhury R, Troup J, Voortman T, Kunutsor S, Kavousi M, Oliver-Williams C, Muka T (Juni 2016). "Use of Plant-Based Therapies and Menopausal Symptoms: A Systematic Review and Meta-analysis". JAMA. 315 (23): 2554–63. doi:10.1001/jama.2016.8012. PMID 27327802.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

[[Category:Magonjwa]]