Mtumiaji:Lucas559/Ugonjwa wa kifo cha ghafla cha watoto wachanga
Lucas559/Ugonjwa wa kifo cha ghafla cha watoto wachanga | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Magonjwa ya watoto |
Dalili | Kifo cha mtoto chini ya umri wa mwaka mmoja[1] |
Miaka ya kawaida inapoanza | Ghafla[1] |
Visababishi | Haijulikani[1] |
Sababu za hatari | Kulalia tumbo au upande, kupata joto kupita kiasi, kuathiriwa na moshi wa tumbaku, kushiriki kitandani[2][3] |
Njia ya kuitambua hali hii | Hakuna sababu iliyopatikana baada ya uchunguzi na uchunguzi wa maiti[4] |
Utambuzi tofauti | Maambukizi, matatizo ya kijeni, matatizo ya moyo, unyanyasaji wa watoto[2] |
Kinga | Kuwalaza chali watoto wachanga, viboreshaji, kunyonyesha, chanjo[5][6][7] |
Matibabu | Usaidizi kwa familia zilizoathirika[2] |
Idadi ya utokeaji wake | 1 in 1,000–10,000[2] |
Ugonjwa wa mtoto mchanga kufa ghafla (kwa Kiingereza Sudden infant death syndrome; kifupi: SIDS) unaleta kifo cha ghafla kisichoelezeka cha mtoto wa chini ya mwaka mmoja.[1] Utambuzi wake unahitaji kwamba kifo hicho kibaki bila kuelezewa hata baada ya uchunguzi wa kina wa maiti na uchunguzi wa kina wa eneo la kifo.[4] SIDS hutokea mara nyingi wakati wa usingizi.[2] Kwa kawaida, kifo hutokea kati ya saa 00:00 na 09:00 [8] na kwa kawaida hakuna kelele au ushahidi wa kupambana.[9]
Sababu halisi ya SIDS haijulikani.[3] Limependekezwa sharti la kuwepo mchanganyiko wa mambo ikiwa ni pamoja na uwezekano mahususi wa kuathiriwa, wakati mahususi katika kukua na shinikizo la kimazingira.[2][3] Shinikizo hizi za kimazingira zinaweza kujumuisha kulalia tumbo au upande, joto kupita kias na kuathiriwa na moshi wa tumbaku.[3] Kukosa hewa kwa bahati mbaya kutokana na kushiriki kitandani (pia hujulikana kama kulala pamoja) au vitu laini vinaweza kuchangia.[2][10] Sababu nyingine ya hatari ni kuzaliwa kabla ya wiki 39 za ujauzito.[7] SIDS huchangia takriban 80% ya vifo vya watoto wachanga vya ghafla na visivyotarajiwa (SUIDs).[2] Asilimia nyingine 20 ya hali zake mara nyingi husababishwa na maambukizo, matatizo ya kijeni na matatizo ya moyo.[2] Ingawa unyanyasaji wa watoto kwa njia ya kuwakosesha hewa kimakusudi unaweza kutambuliwa kimakosa kama SIDS, hili linaaminika kuchangia chini ya 5% ya visa.[2]
Njia bora zaidi ya kupunguza hatari ya SIDS ni kumlaza chali mtoto wa umri wa chini ya mwaka mmoja wakati wa usingizi.[7] Hatua zingine ni pamoja na kutumia godoro dhabiti iliyotenganishwa lakini iliyo karibu na walezi, kutokuwepo matandiko yaliyolegea, mazingira ya kulala yenye ubaridi kiasi, kutumia titibandia na kuwaepusha mbali na kuathiriwa na moshi wa tumbaku.[5] Kunyonyesha na chanjo pia vinaweza kuwa kinga.[5][6] Hatua ambazo hazijaonyesha kuwa muhimu ni pamoja na vifaa vya kuweka watoto sawasawa na vichunguzi.[5][6] Ushahidi hautoshi juu ya matumizi ya feni.[5] Msaada wa kuziliwaza familia zilizoathiriwa na SIDS ni muhimu, kwani kifo cha mtoto mchanga ni ghafla na hakina mashahidi, na mara nyingi huhusishwa na uchunguzi.[2]
Viwango vya SIDS hutofautiana karibu mara kumi katika nchi zilizoendelea kutoka moja kati ya elfu moja hadi moja kati ya elfu kumi.[2][11] Ulimwenguni kote, ugonjwa huu ulisababisha vifo vipatavyo 19,200 mwaka wa 2015, na idadi hii ikawa imeshuka chini ya vifo 22,000 vilivyotokea mwaka wa 1990.[12][13] SIDS ilikuwa sababu kuu ya tatu ya vifo kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja nchini Marekani katika mwaka wa 2011.[14] Ugonjwa huu ndio sababu ya kawaida zaidi ya kifo kwa watoto wa umri wa kati ya mwezi mmoja na mwaka mmoja.[7] Takriban 90% ya hali zake hutokea kabla ya umri wa miezi sita, na hutokea mara nyingi kati ya miezi miwili na miezi minne.[2][7] Vifo hivi ni kawaida zaidi kwa wavulana kuliko wasichana.[7] Viwango vyake vimepungua katika maeneo yenye "kampeni za usingizi salama" kwa hadi 80%.[11]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Sudden Infant Death Syndrome (SIDS): Overview". National Institute of Child Health and Human Development. 27 Juni 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 Kinney HC, Thach BT (Agosti 2009). "The sudden infant death syndrome". The New England Journal of Medicine. 361 (8): 795–805. doi:10.1056/NEJMra0803836. PMC 3268262. PMID 19692691.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 "What causes SIDS?". National Institute of Child Health and Human Development. 12 Aprili 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 "Centers for Disease Control and Prevention, Sudden Infant Death". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 18, 2013. Iliwekwa mnamo Machi 13, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Moon RY, Fu L (Julai 2012). "Sudden infant death syndrome: an update". Pediatrics in Review. 33 (7): 314–20. doi:10.1542/pir.33-7-314. PMID 22753789.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 6.0 6.1 6.2 "How can I reduce the risk of SIDS?". National Institute of Child Health and Human Development. 22 Agosti 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 7.5 "How many infants die from SIDS or are at risk for SIDS?". National Institute of Child Health and Human Development. 19 Novemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Optiz, Enid Gilbert-Barness, Diane E. Spicer, Thora S. Steffensen; foreword by John M. (2013). Handbook of pediatric autopsy pathology (tol. la Second). New York, NY: Springer New York. uk. 654. ISBN 9781461467113. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 15 Septemba 2017.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Scheimberg, edited by Marta C. Cohen, Irene (2014). The Pediatric and perinatal autopsy manual. uk. 319. ISBN 9781107646070. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 15 Septemba 2017.
{{cite book}}
:|first=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ "Ways To Reduce the Risk of SIDS and Other Sleep-Related Causes of Infant Death". NICHD. 20 Januari 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 2 Machi 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 11.0 11.1 Duncan, Jhodie R.; Byard, Roger W. (2018), Duncan, Jhodie R.; Byard, Roger W. (whr.), "Sudden Infant Death Syndrome: An Overview", SIDS Sudden Infant and Early Childhood Death: The Past, the Present and the Future, University of Adelaide Press, ISBN 9781925261677, PMID 30035964, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Julai 2020, iliwekwa mnamo 2019-08-01
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ GBD 2013 Mortality Causes of Death Collaborators (Januari 2015). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 385 (9963): 117–71. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMC 4340604. PMID 25530442.
{{cite journal}}
:|last=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Wang, Haidong; Naghavi, Mohsen; Allen, Christine; Barber, Ryan M.; Bhutta, Zulfiqar A.; Carter, Austin; Casey, Daniel C.; Charlson, Fiona J.; Chen, Alan Zian (Oktoba 2016). "Global, regional, and national life expectancy, all-cause mortality, and cause-specific mortality for 249 causes of death, 1980-2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1459–1544. doi:10.1016/s0140-6736(16)31012-1. PMC 5388903. PMID 27733281.
{{cite journal}}
: Invalid|display-authors=29
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hoyert DL, Xu JQ (2012). "Deaths: Preliminary data for 2011" (PDF). National Vital Statistics Reports. 61 (6): 8. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-02-02.
[[Category:Magonjwa]]