Nilizaliwa Marekani, lakini Tanzania ni kwangu moyoni. Baada ya kuanza kujifunza Kiswahili kwa ajili ya kazi, nilikaa Tanzania kwa miaka mingi. Nilipewa kiwanja na nikajenga nyumba Iringa kijijini. Siku hizi ni lazima niwepo Marekani tena kufanya kazi, lakini narudi Bongo kila nikiwa na nafasi. Ukijikuta karibu na Malangali Sekondari, utaona mlima ng'ambo ya mto mdogo. Kwenye mlima utaona nyumba ya vigae. Vuka mto, panda mlima, na ukifika kwenye nyumba, bisha hodi. Kama mimi nipo nyumbani, itabidi ukae - kuna ugali sasa hivi...