Mtumiaji:Muddyb/Mkude Simba

Mkude Simba

Mkude Simba
Amezaliwa Mussa Yusufuph Mahenge
(1986-12-30)Desemba 30, 1986 Mahenge, Morogoro, Tanzania
Morogoro
Jina lingine Kitale, Teja, Bwakila
Kazi yake Mwigizaji, mwigizaji wa sauti, mwimbaji
Miaka ya kazi 2002
Ndoa Fatma Abbas
Watoto 2

Mussa Yusufuph Mahenge (amezaliwa 30 Disemba 1986) ni mwigizaji, mwongozaji na mwandishi wa muswada andishi wa filamu kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa uhusika wake wa Kitale ambao hucheza kama mraibu wa dawa za kulevya (teja) na Mkude Simba[1] kupitia vitangazo vidogo vya EFM Radio. Mbali na uigizaji, Kitale vilevile ni mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava). Mwaka wa 2010, alitoa Hili Dude Noma akimshirikisha Corner na Midezoo, Mbuzi Kagoma Kwenda (2012), akimshirikisha Canaltop na Sharo Milionea, Nawaektia (2014) akimshirikisha Midezoo, Mithuni Chakraboty (2019).

Alianza kufahamika katika kundi la Kaole Sanaa Group kabla ya kuhamia rasmi Fukuto Arts Group la Tuesday Kihangala kati ya 2002/2003. Kwa Kihangala alifanya Rangi ya Chungwa (2003), Jumba la Dhahabu na Ua Jekundu.

Baadaye akatengeneza filamu zake mwenyewe ikiwa ni pamoja na Mbwembwe, Kubwa Jinga, Porojo, Bad Night na More Than a Lion.

Maisha ya awali

hariri

Mkude alizaliwa na jina la 'Mussa Yusuph Mahenge' alizaliwa mnamo 30 Disemba 1986[2] huko mkoani Morogoro kwa baba na mama wote Walugulu. Alisoma katika shule ya msingi Tandale Uzuri, Dar es Salaam na kuhitimu 2001. Katika familia yao wapo sita, watano wamezaliwa baba na mama mmoja, Kitale wa kwanza--vilevile wa pili kwa upande wa baba kwa sababu alizaa mtoto wa kike kabla ya kumuoa mama'ke Kitale.

Kitale alianza kuigiza tangu akiwa Shule ya Msingi Uzuri. Alijiunga na Kaole Sanaa Group mnamo 2002. Kipindi angali anaishi Manzese, aliishi karibu na waigizaji maarufu wa kundi la Kaole, Abdallah Mkumbila (Muhogo Mchungu) na akina Swebe Santana. Nyakati hizo, alitamani sana kuigiza baada ya kuwaona walichokuwa wakikifanya. Alivyojiunga Kaole, alikutana na Tuesday Kihangala. Kupitia huyu, ilikuwa rahisi kufanya kazi Kaole. Tues na Mkude wanatoka kijiji kimoja huko Morogoro.

Kukatokea mfarakano baina ya Kihangala na kiongozi mkuu wa kundi la Kaole kipindi hicho Bwana Christian Muhenga na hatimaye Tues akatoka na kuanzisha kundi lake la maigizo maarufu kama 'Fukuto Arts Group' akamchukua na Mkunde Simba. Akiwa huko, alishiriki katika tamthiilia ya Rangi ya Chungwa, Ua Jekundu na Jumba la Dhahabu kabla ya kwenda kufanya kazi za kujitegemea.

Filamu za kujitegemea

hariri

Mkude alianza kuandika filamu zake mwenyewe mnamo mwaka wa 2009. Filamu ya kwanza ilikuwa Badnight. Zifuatazo ni filamu alizoandika na kuziongoza;


  1. Badnight - 2009
  2. Mwembwe - 2009
  3. More Than a Lion - 2010
  4. Porojo - 2013
  5. Chizi Kalogwa Tena - 2014
  6. Harusi ya Teja - 2015
  7. Stan Bakora - 2019
  8. Mzee Ndigula - 2019
  9. Kimbiji- 2019
  10. Mkubwa Bure - 2019

Mbali na filamu, Mkude pia alitoa tamthilia maarufu nchini Tanzania - Maneno ya Kuambiwa. Tamthilia inarushwa kupitia TV ya E-TV na idhaa yake ya YouTube ya Mkude Simba.

Orodha ya filamu alichocheza

hariri
  1. Chizi Kalogwa Tena
  2. 4 Days Mission
  3. Sina Jinsi
  4. Mkweli Nani
  5. Dini Imani
  6. Msela
  7. Utani
  8. Zungusha
  9. Bwege Mtozeni
  10. Break Down
  11. Shoe Shine
  12. Street Girl
  13. Chips Kuku
  14. Zungu la Unga
  15. Lakuchumpa
  16. More than a Lion
  17. Porojo
  18. Mpela Mpela
  19. Utanibeba
  20. Jumba la Dhahabu Season 1
  21. Vituko Show Vol. 10
  22. Sons & Jobs
  23. Mission Town
  24. Simu ya Kichina
  25. Alosto
  26. Back from New York

Marejeo

hariri
  1. https://www.youtube.com/watch?v=dCorrCZE3ns
  2. "Musa Kitale 'Kitale' | Actor, Commedian, Singer, — Bongo Movies - Buy Tanzania Movies and DVD's Online". www.bongocinema.com. Iliwekwa mnamo 2020-02-16.