Je, wajua chochote kuhusu mkoa wa mbeya?

Je, ulishawahi kutembelea mkoa huo?

Mbeya ni mkoa unaopatikana magharibi mwa Tanzania, kanda ya kusini (Nyanda za juu), ikiwa mkoa huo ni mkoa wa nne kwa ukubwa nchini.

Mkoa huo ulipewa cheo na kua jijji. Wengi wa wakazi wake ni wakulima.

Mbeya Kuna makabila Kama wanyakyusa ambao ndio wazawa, wasafwa ambao walikua Kama wakimbizi wa mkoa huo wakati wa ukoloni, na makabila mengine ya mpakani Kama wangoni upande wa Malawi na wanyamwanga walioko mkoa wa songwe ambao zamani ilikua ni wilaya mojawapo ya mkoa wa mbeya.

Mkoa huo una mandhari nzuri sana hasa kwa kupigia picha, ku-shoot video na mandhari ya kupumzikia kwa ujumla. Wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili Tanzania wametoka katika mkoa huo, akiwemo Mwasongwe, Mwahangila na wengine wengi. Na pia hata kwa upande wa bongo flavor, wapo wasanii ambao wametoka katika mkoa huo, akiwemo Rayvanny(Raymond mwakyusa), Izzo business (Mbeya boy) na wengine wengi.

Karibu Sana mbeya ardhi ya shibe💁.