Isaac newton Isaac Newton ni mwana hisabati,phizikia,na mwana tekinologia kutoka wingereza aliyezaliwa mwaka 1643 alisoma chuo cha cambridge.Anatambulika kama mwanasayansi mwenye ushawishi mkubwa katika mapinduzi ya kisayansi.Katika kitabu chake cha hisabati ya falsafa ya asili ambayo ilichapishwa mwaka 1687,katika kitabu hicho aliandika sheria za mvutano na mwendo wa dunia ambayo ilishanngaza wanasayansi wengi,pia aliunda darubini ya kwanza inayoonesha matendo mbalimbali ya kisayansi.Pia alikuwa mkristo mcha MUNGU lakini alikataa fundisho la utatu mtakatifu,isaac newton kabla ya kufa alishawahi kuwa mbunge wa chuo cha cambridge.akafa mwaka 1727.Hii ndio historia yake kwa ufupi.