Nimezaliwa January 20 1993, katika. kijiji cha Kagugu, kata ya Kagugu, jimbo la uchaguzi la Mbinga mjini, Wilaya ya Mbinga ,mkoa wa Ruvuma. Baba yangu ni Mzee Adrieno Sebastian Mapunda na Mama ni Ostina John Kawonga. Lugha mama ni  Kimatengo. Pia naongea kiingereza na Kiswahili.

Nilizaliwa katika familia ya wakulima.Babu yangu Mzee Sebastian Mapunda (Ndomondo) alikuwa mkulima akitokea Katika Ukoo wa Jumbe Kasuma. Katika familia ninao Ndugu wengine kadhaa, nikiwa na Dada watatu na kaka Mmoja. Familia yangu ilikuwa ni ya watoto Sita. Mmoja Alifariki mwaka 2007 Akiwa Shule ya Secondary ya Mbangamao kidato cha Kwanza.

Miaka 2000 – 2006  nikasoma Shule ya Msingi huruma, halafu 2007  – 2010 Sekondari ya Makita iliyopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma na 2011 - 2013 Hagafilo high school huko Njombe.

Kuanzia mwaka 2013 nilisoma Uhasibu  katika Chuo cha Uhasibu Tanzania Tawi la Mbeya nikapata Stashahada yangu ya kwanza mwaka 2016. Mwezi wa October mwaka huo nikafanya kazi Katika Office za Halimashsuri ya Mbinga kama mhasibu wa kujitolea. Mwezi November nilikwenda Mbeya kwa Mapumziko kidogo ambapo nilirejea mwezi Mach 2017, Nikaendelea na kazi Katika Halimashsuri hapo kwa Muda mfupi sana wa mwezi mmoja. Baada ya Hapo nikapata kazi Katika kituo cha Afya cha Mt. Vincent Kilichopo Mbinga Mjini.

Tarehe 11/08 /2019 nilimposa Binti Emilliana Ndomba kuwa Mchumba wangu. Na Tarehe 7/08/2019 nilikwenda naye kijijini kwetu Kagugu kwa Lengo la kumtambulisha kwa Wazazi na Ndugu wengine. Nashukuru sana Mungu mambo yalikwenda Vizuri sana kama yalivyopangwa. Nashukuru Wazazi wetu na Ndugu walitupokea Vizuri sana.

Niliposoma Shule ya Msingi huruma niliteuliwa kuwa kiongozi wa taaluma nikisimamia pia michezo, Nikiwa Shule ya Sekondari ya Makita nilichaguliwa kuwa kiongozi wa Starehe na Maafa, Nilipokuwa Chuo cha Uhasibu niliteuliwa na Rais wa Chuo kuwa Mbunge wa bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Chuo TIASO.  Ninao Marafiki kadha wa kadha, Rafiki yangu mkubwa anaitwa Chama George Kaume. a.k.a Cg. Na wengine wengi. Nawashukuru sana Marafiki zangu kwani mmekuwa msaada mkubwa na wamekuwa karibu sana nami. Mfano Christoms Ndunguru yeye ni kama Ndugu yangu na Mtu wa karibu sana kwangu na pia ni kama Mshauri wangu mkubwa sana.

Kuna mtu anaitwa Aron Nsajigwa wa Dar Es Salaam, Ni mtu poa Sana yeye ni Rafiki yangu na ni msaada wangu mkubwa sana kipindi nipo Chuoni kuanzia Mwaka 2013 Hadi 2016.

Kuna mtu anaitwa Christian Msuha wa Maguu Mbing, yeye ni Rafiki yangu pia na nilikuwa nakaa naye chumba kimoja Chuoni.

Kuna mtu anaitwa Silyvester Dyson Yobele (CR) wa Dar Es Salaam yeye ni Mbunge Mwenzangu kipindi nipo Chuo. Vilevile ni Padre mtarajiwa namwombea sana kwa Mwenyezi Mungu atimize malengo yake ya kumtumikia yeye.

Nashukuru sana watu wangu Mungu awabariki kwelikweli. Tuendelee kuombeana.