Mulatu Astatke
Mulatu Astatke (alizaliwa Jimma, 19 Desemba 1943) ni mwanamuziki na mtunzi kutoka Ethiopia anayefahamika kama baba wa Ethio-Jazz (pia unaitwa Tizita au Tezeta).
Mulatu alisoma muziki London, New York City, na Boston, ambapo alijifunza kuunganisha muziki wa Jazz na muziki wa Kilatini pamoja na muziki wa Kiethiopia. Mulatu ni mwanzilishi wa kupiga vibraphone na ngoma ya konga katika muziki wa Ethiopia, na anapiga pia ngoma mbalimbali, na vinanda mbalibali. Albamu zake zinalenga muziki wa ala, na Mulatu anatokea kwenye albamu zote tatu zilitolewa wakati wa kipindi cha dhahabu cha Ethiopia cha miaka ya 1970[1].
Maisha ya Mwanzoni na Kazi
haririWakati alipokuwa mdogo mwishoni mwa miaka ya 1950, familia yake ilimpeleka Wales ili ajifunze uhandisi. Hata hivyo, Mulatu alianza kujifunza muziki badala ya uhandisi katika Chuo cha Lindisfarne, na hatimaye kupata shahada ya muziki kutoka Chuo cha Trinity huko London. Katika miaka ya 1960, Mulatu alisafiri Marekani kwa hiyo aliweza kuendelea na masomo yake katika Chuo cha Berklee mjini Boston. Halafu, katika miaka ya 1966 katika New York, Mulatu alirekodi na kutoa albamu zake mbili za kwanza, Afro-Latin Soul, Vol. 1&2. Albamu hizi zilionyesha Mulatu akipiga vibraphone pamoja na piano na ngoma ya konga, ambayo ilikuja kuwa mtindo wake. Katika miaka ya 1970, Mulatu aliupeleka mziki wake Ethiopia, na alishiriki katika kazi pamoja na wanamuziki maarufu kama Frank Holder, Mahmoud Ahmed, Duke Ellington, na Hailu Mergia[2].
Mulatu alirekodi pia Mulatu of Ethiopia (1972), Yekatit Ethio Jazz (1974), na Tche Belew (1977) (pamoja na Walias Band) wakati wa miaka ya 1970. Hata hivyo, wakati wa miaka ya 1980, muziki wake ulisahaulika nje ya Ethiopia. Hatimaye, wakati wa miaka ya 1990, muziki wa Mulatu uligunduliwa tena na ilikuwa maarufu sana katika Marekani kwa sababu ya kutolewa kwa Ethiopiques Volume 4: Ethio-Jazz & Musique Instrumentale 1964-1974. Albamu hii ilileta muziki wake kwa watazamaji wa kimataifa. Wakati wa miaka ya 2000 na 2010, Mulatu alishirikiana kazi pamoja na Either/Orchestra, The Heliocentrics, na Black Jesus Experience, na miziki yao yote iliheshimika kama miziki ya jadi ya Ethiopia[3][4].
Katika 2008, Mulatu alipomaliza kufanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Harvard, alifanya kazi ya kubadilisha vyombo vya muziki vya jadi ya Kiethiopia kwenye vyombo vya muziki wa kisasa. Mulatu pia ameheshimiwa na Chuo Kikuu cha MIT na alitunukiwa shahada ya uzamivu ya heshima kutoka Chuo cha Berklee[5][6].
Rekodi za muziki
haririKama msanii mwenyewe
hariri- Maskaram Setaba, 7’’ (1966)
- Afro-Latin Soul, Vol. 1 & 2 (1966)
- Mulatu of Ethiopia (1972)
- Yekatit Ethio-Jazz (1974)
- Plays Ethio-Jazz (1989)
- Mulatu Astatke
- Assiyo Bellema
- Ethiopiques Volume 4: Ethio-Jazz & Musique Instrumentale, 1964-1974 (1998)
- Mulatu Steps Ahead with the Either/Orchestra (2010)
- Sketches of Ethiopia (2013)
Kama msanii mshiriki
hariri- Ethiopian Modern Instrumental Hits (1974)
- Tche Belew with Hailu Mergia & The Walias Band (1977)
- New York – Addis – London: The Story of Ethio-Jazz 1965-1975
- The Rough Guide to the Music of Ethiopia (2004)
- Broken Flowers (2005)
- Inspiration Information with The Heliocentrics (2009)
- Cradle of Humanity with Black Jesus Experience (2016)
- To Know Without Knowing with Black Jesus Experience (2019)
Tanbihi
hariri- ↑ "Lost Funk Masterpieces Of Ethiopia". NPR.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
- ↑ "Ethio Jazz | Ethiopian Jazz Music". web.archive.org. 2013-08-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-08-29. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
- ↑ "Jazz | AllAboutJazz.com". web.archive.org. 2010-04-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-04-21. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
- ↑ "Mulatu Astatke, the father of Ethiopian jazz", The Economist, 2010-10-22, ISSN 0013-0613, iliwekwa mnamo 2019-07-25
- ↑ "Eagles, Alison Krauss, Mulatu Astatke Receive Honorary Degrees at Commencement | Berklee College of Music". www.berklee.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
- ↑ Culshaw, Peter (2010-03-24), Mulatu Astatke: the lounge lizard of counterpoint (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0307-1235, iliwekwa mnamo 2019-07-25
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mulatu Astatke kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |