Mvuke
Mvuke hutaja maji yaliyoingia katika hali ya gesi lakini inaweza kutaja gesi yoyote iliyotokana na kiowevu kama kinaongezeka joto. Badiliko la kiowevu kuwa mvuke huitwa uvukizaji.
Kwa kawaida tunaita "mvuke" ya maji unaoonekana kama moshi mweupe unaopanda juu ya uso wa maji yanayopashwa moto. Lakini kwa macho ya fizikia hii si mvuke halisi bali mchanganyiko wa matone madogo ya maji na hewa. Mvuke kamili haionekani.
Mvuke hushika nishati ndani yake ambao ni umbo badili la nishati ya joto iliyobadilisha maji (au kiowevu kingine) kuwa mvuke. Hapo ndipo msingi wa kutumia nguvu iliyopo ndani ya mvuke kwa kufanya kazi kwa mfano kwa njia ya injini ya mvuke.