Nishati inamaanisha uwezo wa kufanya kazi na kusababisha mabadiliko. Katika sayansi nishati hupimwa kwa kipimo cha SI joule.

Nishati
Umeme wa radi ni uvunjiko wa nguvu za kiumeme katika hewa unaotokana na uwindi umeme mkali (kutoka nishati uweza kiumeme na kuwa nishati ya kimakanika ya mwendo ovyo wa kimolekyuli (kusuguana na kufanya ngurumo, joto, na mwanga).
Alama za kawaida
E
Kizio cha SIJouli
Kwavizio msingi vya SIJ = kg⋅m2⋅s−2

Katika sayansi ina mtazamo wa pekee. Ni aina ya kani/nguvu/uwezo ambapo kazi ikifanyika kama kusogeza kitu, basi tunasema nishati imetumika.

Aina za nishati

hariri

Aina hizi hutegemea matumizi na mabadiliko yake; k.m. kuna:

  • 1. Nishati ya jua
  • 2. Nishati ya mwanga
  • 3. Nishati ya joto
  • 4. Nishati ya umeme
  • 5. Nishati ya kikemikali
  • 6. Nishati ya kimakanika
  • 7. Nishati ya sumaku
  • n.k.

Aina za nishati hutokana na asili au chanzo chake. Zifuatazo ni baadhi yake:

Makundi ya Nishati

hariri

Nishati huwekwa katika makundi kulingana na matumizi ya mwanadamu na ukubwa wa uhitaji wake katika sura ya kijamii, halafu pia na aina ya matumizi.

Nadharia juu ya nishati

hariri

Fizikia hueleza nishati na tabia zake kimaumbile na msababisho kimatukio. Nayo hutaja kama nadharia; kufafanua mienendo.

Ufafanuzi

hariri

Ni nguvu iwezeshayo kazi kufanyika.

Kazi, kifizikia, ni kitendo kinachohusisha mabadilishano ya namna moja ya nishati hadi nyingine, ama pia kubadili hali ya kimaumbile na nafasi. Kwa mfano, kusogeza kiti ni kazi inayojidhihirisha kwa kuhamisha kiti toka sehemu moja hadi nyingine.

Kizio cha kazi ni Juli.

Tathmini ya kihesabu ya kazi kulingana na nishati kifizikia hukokotolewa kwa thamani ya Juli na kadhaa.

Hali kuu mbili

hariri

Hujidhihirisha katika sura mbili na kutathminiwa hivi:

  • Nishati Uweza
  • Nishati Mwendeko

Nishati Uweza

hariri

Hii ni hali ya kiutathmini uwezo wa nishati kufanya kazi ama kuleta zao fulani la kikazi katika wakati ambao tukio halisi halijatendeka. Kama jiwe juu ya kigingi cha mlima kabla halijadondoka lina tathmini ya uwezo wa nguvukazi sawa na mara litakapofika chini wakati wa kudondoka.

Nishati Mwendeko

hariri

Hii ni hali ya kutathmini uwezo wa nishati kufanya kazi endelevu kiwakati. Kama Jiwe lililorushwa lina nguvukazi alhali likipea.

Kanuni ya Uhifadhi Sawia wa Nishati

hariri

Hii ni kanuni inayoelezea mbadilishano wa nishati kutoka hali moja hata nyingine; nayo inasema: Nishati haiwezi kujengwa wala kubomolewa bali hubadilika kutoka hali moja hadi nyingine.

Hii ni kusema kuwa, kiasi cha nishati kitumikacho kufanya kazi huwa sawa sawa na kiasi cha kazi kiutathmini. Hivyo kama kitendo kinaweza kurudishwa kilikotekea, kiasi kile kile cha nishati itapatikana.

Vile vile nishati inaposababisha tukio ambalo nishati za aina nyingine kutukia, basi kiasi cha tathmini yake ni sawa sawa na nishati iliyosababisha.

Mifumo perepetua ya kimakanika

hariri

Mfano wa kanuni hii unaonekana kwenye bembea kama ile kwenye saa ya ukutani ya kimakanika. Jiwe la kuning'inia linapofika usawa wa juu kabisa; huwa na nishati uweza ya juu kabisa. Halafu Nishati Mwenendo huwa ni sifuri pale linapokuwa limesimama kabla ya kubembea na kurudi chini. Katika hali ya wima kabisa, nishati uweza huwa ni sifuri na wakati nishati mwenendo huwa juu kabisa. Na hivyo kufanya mabadilishano ya Nishati Uweza na Nishati Mwenendo vinavyohusiana katika mifumo ya kazi za kimakanika.

Changamoto ya Nadharia ya Uhifadhi Sawia wa Nishati

hariri

Kanuni hii katika nyanja ya kifizikia imefika njia panda baada ya mifumo mpya wa uzalishaji nishati kugunduliwa.

  Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nishati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.