Mwanangu Nakuusia ni utendi mrefu wa Kiswahili ulioandikwa na mwandishi Audax Kahendaguza Vedasto mwaka 1994 lakini ukaja kuchapishwa mwaka 2009.

Utenzi huu ulikuwa ukizungumzia wosia ambao muandishi alikuwa akimuusia mtoto wake namna ya kuishi Duniani katika maisha ya kawaida na maisha ya kiroho. Ni utenzi ambao uliwagusia mtoto wa kike na mtoto wa kiume kwa wakati mmoja [1]

Utenzi huo wenye jumla ya beti mia saba hamsini na saba, umeanza mtunzi akiwa amekaa na mwanae ambaye ni wa kike na yule wa kiume huku amsihi atulie ili apewe wosia ambao utamuangazia kuhusu dunia ambayo inahitaji akili nyingi ili kuishi salama na mwisho anamalizia kwa kujieleza wasifu wake kama baba na mtunzi ndani ya utenzi huu.

Tanbihi hariri

  1. Vedasto, Audax Kahendaguza. ([2009]). Mwanangu nakuusia. Dar es Salaam, Tanzania: Idea International Publishers. ISBN 9789987922031. OCLC 445489459.  Check date values in: |date= (help)
  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanangu Nakuusia kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.