Mwele Ntuli Malecela

Mwele Ntuli Malecela (26 Machi 1963 - 10 Februari 2022) alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI)[1]. Aliwania nafasi ya mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.[2][3] Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikuwa akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa Afrika kama msimamizi wa masuala ya utawala, sera na ushauri wa kidiplomasia.

Mwele Ntuli Malecela
Tarehe ya kuzaliwa 26 Machi 1963
Tarehe ya kifo 10 Februari 2022
Chama CCM
Digrii anazoshika Shahada ya uzamivu
Kazi Mkurugenzi wa Taasisi ya tafiti za kiafya (NIMRI)


Maisha ya awali na kazi hariri

Baada ya kuhitimu shahada ya kwanza katika masuala ya wanyama katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam[4] alijiunga na taasisi ya tafiti za kiafya (NIMRI) mnamo mwaka 1987. Katika kipindi hicho Mwele alifafanya tafiti za ugonjwa wa homa ya matende katika kituo cha Amani.

Baada ya hapo aliendelea na elimu ya juu katika chuo kiitwacho London School of Hygiene and Tropical Medicine ambako alitunukiwa shahada yake ya pili mwaka 1990 na shahada ya uzamivu mwaka 1995. Aliendelea na tafiti zake katika taasisi ya NIMRI mpaka kufikia mwaka 1998 ambapo alipewa cheo cha mkurugenzi wa tafiti. Mwaka 2000 Mwele alikua kiongozi wa program ya homa ya matende, ambayo imekua ikifanya kazi katika wilaya takribani 53.

Maisha ya kisiasa hariri

Malecela alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) mnamo mwaka 1981 alipokuwa Kilakala. Kwa wakati huo alihitajika kupata mafunzo maalumu kwanza kabla ya kujiunga na chama. Dokta Malecela alifanya mafunzo hayo mwezi Aprili 1981[5] na baada ya hapo amekuwa mwanachama wa kudumu hadi kufikia sasa.

Marejeo hariri

  1. Mwele Malecela on Tanzania, IANPHI-Africa, and being a woman leader in Public Health. ianphi.org. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-09-24. Iliwekwa mnamo 2018-06-20.
  2. Meet the staff Mwelecele Ntuli. nimr.or.tz. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 2018-06-20.
  3. News events East africa July 2013. lshtm.ac.uk. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2018-06-20.
  4. Director general of the National Institute for Medical Research in Tanzania and is the first woman to hold this position.. ianphi.org.
  5. Presidential hopefuls on CCM ticket broadens democracy. dailynews.co.tz. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-05-06. Iliwekwa mnamo 2018-06-20.