Nana Gichuru

Mwigizaji wa Kenya

Ephex Kanana Gichuru (alijulikana kwa jina la Nana Gichuru[1]; 14 Disemba 1986[2][3] – 22 Septemba 2015) alikuwa mwigizaji na muendesha vipindi vya televisheni nchini Kenya.

Kama muigizaji, alijulikana kwa uhusika wake katika maonyesho ya televisheni kwa majina ya Noose of Gold, Demigods na How to Find a Husband.[4] Kama mtangazaji, alitakiwa aelezee kipindi cha Interior Designs, maonyesho ya uhalisia ya ki Kenya, kabla ya kifo chake. Pia alikuwa ni miongoni mwa wafanyakazi katika shirika la ndege la nchini kenya. Aliolewa na Richard Wainaina.

Kazi hariri

Gichuru alianza kuzalisha filamu kama Noose of Gold mwaka 2010 na Demigods mwaka 2011. Kazi zake za hivi karibuni katika Uchekeshaji ni How to Find a Husband na onyesho la ukweli Interior Designs

Kifo hariri

Takriban majira ya saa 4 asubuhi, 22 Septemba mwaka 2015, Nana alikua akisafiri ndani ya gari lake aina ya BMW, alipofika makutano ya barabara ya Utawala, aligonga lori na kufa papo hapo. Alikufa akiwa na miaka 28.[5] Kifo chake kilitokea siku kumi baada ya yeye mwenyewe kujitabiria kifo kupitia kurasa zake za kijamii.[6][7] Ibada ya kumbukumbu ya kifo chake ilifanyika tarehe 30 Septemba 2015 katika kanisa la Ruaraka Methodist Church.[8] Alizikwa tarehe 2 Oktoba 2015 nyumbani kwao Kaaga, Meru.

Filamu hariri

Mwaka Kichwa Jukumu Vidokezo Mtandao
2010 – Noose of Gold Felma Wahusika Wakuu NTV
2011 – 12 Demigods Juliana Wahusika Wakuu
2015 How to Find a Husband Wahusika wakuu Maisha Magic East
Interior Designs Mhusika mtarajiwa laikini alifariki kabla ya maonyesho kuanza. NTV

Marejeo hariri

  1. "Nana Gichuru's biography". actors.co.ke. Iliwekwa mnamo October 29, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Nana Gichuru's birthdaty". Heka Heka. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 14 December 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "The memorial service for actress and Kenya Airways crew member 28-year-old Kanana (Nana) Gichuru was held on Wednesday September 30, 2015 at Ruaraka Methodist Church in Nairobi". Tuko. Iliwekwa mnamo 14 December 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. "Nana Gichuru films". Actors.co.ke. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-17. Iliwekwa mnamo 14 December 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "Revealed: Actress Nana Gichuru's final moments before tragic accident". sde. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-17. Iliwekwa mnamo 14 December 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. Kamau, Richard (23 September 2015). "She Drove Super fast, Predicted Her Death and Died Yesterday.. The SHOCKING Story of Nana Gichuru". Nairobi Wire. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-17. Iliwekwa mnamo 14 December 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. "Kenyan actress predicts own death, dies a day after". My Joy Online. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-20. Iliwekwa mnamo 14 December 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. Cynthia, Madame (30 September 2015). "The Late Actress Nana Gichuru’s Memorial Service". Mpasho. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-02-14. Iliwekwa mnamo 14 December 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nana Gichuru kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.