Jina
Jina ni neno au maneno ambayo wanapewa watu, wanyama, nchi, vitu n.k. kwa ajili ya utambulisho.
Majina ya watu
haririUtamaduni, kwa njia ya sheria au desturi, ndio unaoratibu namna ya kupanga na kutumia majina ya watu, kwa kawaida tangu kuzaliwa.
Mara nyingi, pamoja na jina binafsi, mtu anatumia pia majina mengine kama vile la ukoo mzima, au la baba na la babu.
Katika nchi na makabila mbalimbali jina linaweza kubadilishwa, kwa mfano wakati wa ibada ya kuingizwa katika dini fulani au katika utawa, au kuongezewa, kwa mfano kutokana na ndoa.
Wasanii kama waimbaji au waandishi mara nyingi hutumia jina la kisanii badala ya jina la kawaida.
Mara nyingine jina linafupishwa, hasa kama ni refu mno, au linapambwa kama kwa kumbembeleza mwenye nalo.
Majina ya wanyama
haririKila aina ya wanyama inapewa jina maalumu la kuwatofautisha na wengine. Mfano: tembo akitajwa jina lake humtofautisha na twiga.
Majina ya nchi
haririKila nchi duniani lina jina lake maalumu ambalo huitambulisha nchi husika pamoja na raia wake.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |