Nancy Lynch
Nancy Ann Lynch (amezaliwa Januari 19, 1948) [1] ni mwanahisabati, mwananadharia, na profesa katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts . Yeye ni Profesa wa NEC na mkuu wa idara ya sayansi ya uhandisi EECS katika Maabara ya Sayansi ya Kompyuta na MIT.
Elimu na maisha ya awali
haririLynch alizaliwa Brooklyn, na alikua na taaluma ya Hisabati. Aliudhuria chuo cha Brooklyn College and MIT, ambapo alihitimu na shahada ya uzamili mwaka 1972 chini ya Albert R. Meyer.
Kazi
haririAlihudumu katika kitivo cha hesabu na sayansi ya kompyuta katika vyuo vikuu vingine kadhaa, ikijumuisha Chuo Kikuu cha Tufts, Chuo Kikuu cha Kusini mwa California, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Florida, na Taasisi ya Teknolojia ya Georgia (Georgia Tech), kabla ya kujiunga na kitivo cha MIT mnamo 1982. Tangu wakati huo, amekuwa akifanya kazi kwa kutumia taaluma yake ya hisabati kutengeneza mifumo mbalimbali.
Bibliografia
haririLynch, Nancy; Merritt, Michael; Weihl, William; Fekete, Alan (1994). Atomic Transactions. San Mateo, California: Morgan Kaufmann. ku. 476. ISBN 9781558601048.
Lynch, Nancy A. (1998). Distributed Algorithms (tol. la 2nd). San Francisco, California: Kaufmann. ISBN 978-1558603486.
Kaynar, Dilsun; Lynch, Nancy; Segala, Roberto; Vaandrager, Frits (2011). The Theory of Timed I/O Automata (tol. la 2nd). San Rafael, California: Morgan & Claypool. uk. 137. ISBN 9781608450039.
Marejeleo
hariri- ↑ Who's who of American women. Marquis Who's Who, 1973. p. 587.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nancy Lynch kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Viungo vya nje
hariri- Ukurasa wa nyumbani wa Nancy Lynch huko MIT
- Works by or about Nancy Lynch )
- Msururu wa mihadhara iliyoalikwa katika PODC 2008 na CONCUR 2008.