'

Nancy Sumari
Nancy akiwa na Mama Salma Kikwete.
Amezaliwa7 Agosti 1986 (1986-08-07) (umri 37)
Arusha
NchiTanzania
Kazi yakeMwanamitindo
TajiMiss Tanzania 2005
NduguNakaaya


Nancy Abraham Sumari (alizaliwa 7 Agosti 1986) alikuwa mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2005 na Mrembo wa Dunia wa Afrika kwa mwaka 2005.

Maisha binafsi hariri

Nancy Sumari alizaliwa mkoani Arusha Tanzania, akiwa mtoto wa tatu katika familia ya Abraham Simango Sumari, akiwa na dada yake Glory aliyekuwa anampa hamasa na ushauri zaidi juu ya masuala ya urembo. Ndugu zake wengine katika ukoo wao ni Devis, Patra, Tumo na Nakaaya Sumari.

Alipata elimu yake ya msingi mjini Nairobi, Kenya katika shule ya msingi ya Blue Bells. Baadaye kuingia elimu ya Sekondari ya wanawake ya Maasai ya huko huko Nairobi ’NBO’ na kuhitimu mwaka 2004 na baadae kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akisomea masuala ya utawala wa biashara.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nancy Sumari kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.